Na Ahmed Abdulla, Zanzibar
Saratani ya shingo ya kizazi ni moja ya maradhi yanayoathiri maisha ya wanawake wengi duniani,hususan katika nchi zinazoendelea.
Kila mwaka maelfu ya wanawake hupoteza maisha kutokana na ugonjwa huu,ingawa kwa kiasi kikubwa unaweza kuzuilika na kutibiwa iwapo utagundulika mapema.
Zaidi ya kuwa ni changamoto ya kiafya lakini pia saratani ya shingo ya kizazi huleta maumivu ya kimwili,kisaikolojia na hata kijamii kwa wanawake na familia zao.
Khadija Kassim Khamisi ni muuguzi na muknga katika hospital ya wilaya Chumbuni wilaya ya Mjini alisema saratani ya shingo ya kizazi mara nyingi haioneshi dalili za haraka hivyo mtu akikosa kupima afya mapema ugonjwa huo unagunduliwa ukiwa umechelewa kwa wale ambao wameshaathirika na maradhi hayo.
Alisema kinga bora ni kufanya uchunguzi wa mara kwa mara na kupata chanjo ya HPV Human Papiloma Virus ili kuweza kuenea kwa ugonjwa huo.
‘’Wanawake wengi hufika hospital wakiwa katika hatua za mwisho za ugonjwa,jambo linaoongeza gharama za matibabu na kupunguza uwezekano wa kupona na wengi wao wanawake wasiojiweza kifedha huathirika zaid’’alieleza Muuguzi Khadija.
Hivyo amewashauri wanawake kuweka utaratibu wa kupima afya zao ili kuepusha madhara makubwa ya maradhi hayo ambayo yanaweza kuepukika.
Pamoja na hayo makala hii ilizungumza na Radhina Saleh Salum mkaazi wa mchomeke mwera wilaya ya magharib ‘A’ alisema kwa mara ya kwanza nilienda kupima afya yangu na kugundulika na viashiria vya saratani ya shingo ya kizazi lakini kwa vile niliwahi nilipatiwa matibabu na kupona.
‘’Nina washauri wanawake wenzangu kutokupuuza afya zao kipimo cha saratani ya shingo ya kizazi ni bure na cha haraka hivyo usisubiri mpk uchelewe kujua hali yako kwani matibabu yake ni makubwa na athari zake nyingi sana’’ alieleza.
Pia makala hii ilizungumza na mume wa Radhia Saleh, Masoud Abdalla Ali alisema mwanamke anapopima mapema afya yake kunamsaidia kuendelea kulea familia yake bila kuathiri na madhara makubwa ya saratani.
‘’Alieleza kuwa wakati mwanamke anaugua saratani ya shingo ya kizazi familia nzima huathirika,watoto hukosa malezi bora huku uchumi ukipungua kwa kiasi kikubwa kutokana na gharama za matibabu yake hii iliathiri baada ya kupata majibu ya mke wangu licha ya kwamba alipata matibabu na kupona.’’
Hatua za kinga uchunguzi wa mapema na upatikanaji wa tiba ni silaha kuu katika vita dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi .
Ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha elimu inafika kwa wanawake wote hasa walioko vijijini ili kuokoa maisha ya wanawake walio wengi ambao wapo hatarini katika ugonjwa huo.
0 Comments