Binaadamu siku zote hutakiwa ajuwe alipo na wapi anataka kwenda. Katika maisha hali hii huwa ni ndoto ambayo hupelekea mtu kupitia mengi , jambo muhimu ni kutokata tamaa na kuendelea kupambana pale unapotaka kwenda. Ingawa unapoteleza au kuanguka unapaswa kuinuka huku ukiendelea na safari ukiwa na matumaini ya siku moja utafika.
Mwaandishi wa Makala hii alifunga safari hadi kwa mwanamke shupavu ,jasiri na mkakamavu anaetamani ndoto yake iweze kutimia .
Nihifadhi Faki Ali mkaazi wa migombani mtoto wa 11 katika familia ya mzee faki yenye watoto 14 mwenye umeri wa miaka 30 yeye ni mwanamke wa kipekee anaepambania familia yake katika harakati zake za maisha na kujishughulisha katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo ikiwemo ujasiriamali wa kufuma vikuba ,pamoja na mtengenezaji wa dalia ya kupambia maiti” Nafanya biashara mbalimbali ambayo inanisaidia kuendesha familia yangu huku nikipata ushirikiano na mama yangu kwa lengo la kijiinua kiuchumi.”Amesema Nihifadhi
licha ya kuwa ni mfanya biashara mwanamke huyo amejishirikisha katika harakati za kugombea nafasi mbalimbali katika chama cha mapinduzi CCM ikiwemo mjumbe wa kamati ya utekelezaji wa tawi la migombani ,mwenyekiti wa ummoja wa vijana wadi ya migombani .” Mnamo mwaka 2017 nikafaikiwa kushika nafasi ya mjumbe wa kamati ya utekelezaji wa wilaya ya mjini huku tukiwa tunapatiwa mafunzo ya uongozi kwa kupitia kamati ya umoja wa vijana ili tuweze kuimarika katika masuala ya uongozi ,kielimu,michezo na kamati hii imewekwa ili tuepuke kuwa tegemezi na kuweza kujishughulisha, vilevile nilisoma suza masuala ya uongozi na nikawa mwenyekiti wa habari pamoja na wa michezo katika serikali ya umoja wa wanafunzi.” Amesema Nihifadhi
Mwaka 2020 aliamua kufanya mamuzi ya kimapinduzi na kugombea nafasi ya uwakilishi katika mkoa wa mjini kupitia viti maalumu kwa vijana .” Baada ya kujiona nimebobea mafunzo ya uongozi pamoja na uzoefu niliokuwa nao nikamua kufanya mamuzi ya kimapinduzi ya kugombea nafsi ya viti maalumu ya vijana katika mkoa wangu wa mjini na katika hatua ya kwanza nilifanikiwa kushinda masikitiko yalikuja katika hatua ya pili wagombea tulikuwa 8 wa mikoa yote Zanzibar na nikafanikiwa kupta nafasi ya nne.” Nihifadhi
Kiukweli mwanamke huyo hakuchoka kuchangamkia fursa aliendelea kugombea nafasi ya Mjumbe wa Baraza kuu Taifa kupitia Ummoja wa Vijana katika mwaka 2022 lakini kwa bahati mbaya hakuweza kufanikiwa kwasababu ya fitina iliongilia kati kwenye uchaguzi huo.”Tulikuwa wagombea 11 huku wajumbe waliopiga Kura ilikuwa zaidi ya 100 changamoto kubwa ya kushindwa ilikuwa watu ambao niliowaaamini ndio waliovunja moyo wangu kwasababu walinizunguka, changamoto nyengine ilikuwa rushwa ya ngono lakini nilijipambambania mwenyewe Kwa kuwatishia nitavujisha tarifa zao ndio ikawa sababu ya kuniogopa.”
Baada ya kupata changamoto hizo ilimfanya kuona siasa sio jambo la lelemama inahitajika kuwa mvumilivu, mkakamavu na kutambua jinsi ya kuishi na maadui zako na kuamua kuenda kujiendeleza elimu ya siasa katika chuo cha Uganda Kwa lengo la kujiandaa na mapambano ya kugombea nafasi nyengine 2025.
Mwanamke huyo alifanikiwa kuwasimamia vijana wenzake kuweza kujiajiri wenyewe na kutotegemea ajira serikalini na kufanikiwa kupata vijana zaidi ya 100 kuweza kujiajiri wenyewe kupitia shughuli mbalimbali ikiwemo ushoni, upambaji, pamoja na ufundi seremala.” Siku zote natamani kuona vijana wezangu wanaweza kujiajiri wenyewe, sikuwa na uwezo wa kuwasomesha vijana wote bali nilitoa mafunzo ya fani yangu ya utengenezaji dalia ya upambaji maiti pamoja na ufumaji vikuba kwa lengo la kuwaasaidia kupata ujuzi ili waweze kujinua kiuchumi.”Amesema Nihifadhi
Mama wa Nihifadhi
Mwanaisha Mgeni amesema ameweza kumruhusu mwanawe kushiriki katika masuala ya uogozi.” Kiukweli mzazi lazima uwe na hofu kumuona mwanao amejihusisha katika mapambano ya kugombea nafasi mbalimbali, kwasababu nafasi hizi zinakuwa na changamoto ikiwemo rushwa ya ngono, hivyo nilikuwa kila kukicha namsihi mwanangu apambane kwa uwezo wake na asikubali kulaghaiwa kwa kitu chochote kwani udhaifu wake ndio kichochezi cha kuzima ndoto zake.” Amesema Mwanaisha
“Vilevile familia yake tumekuwa mstari wa mbele katika kuumuunga mkono kwa kumpa njia mbalimbali za kuweza kumpinga mpinzani wake kwa lengo la kuona ndoto zake pamoja na furaha yake inadumu”.Ameongezea Mwanaisha
Naibu Sheha wa jimbo hilo Mzee Waziri, amesema jinsi anavomtambua mwanamke huyo, kuwa ni mfano wa kuingwa katika jamii ya migombani kwa kujitolea na kuchngamkia fursa mbalimbali za uongozi kwa lengo la kutimiza ndoto zake.”Kijana huyu kwa kiasi kikubwa ameonesha uwezo wake katika kushika nafasiza mbalimbali za uongozi, ikiwemo katika kuboresha hali ya mtaa na kuisaidia jamii katika njia mbalimbali na hii inaonesha juhudi zake za kuwa kiongozi mwenye mchango mkubwa katika jamii.” Amesema Mzee
“Kwa mujibu wa sense ya watu na maaakazi ya mwaka 2022 inaonesha Zanzibar ina watu 1,889,773 kati ya hao wanaume ni 915,492 na wanawake ni 974,281 sawa na asilimia 51.6 ya wakaazi wote Zanzibar .Vijana wanawake 179,581 na wanaume 183,826 , hii inaonesha jumla ya vijana wanawake na wanaume ni 363,407 licha ya wingi wa vijana wetu hao lakini bado kuna upungufu wa kushika nafasi ya uongozi, hivyo inahitaji vijana wakike kupewa mafunzo zaidi ili kuweza kushiriki nafasi mbalimbali za uongozi kwa lengo la kutimiza ndoto zao”. Amesema Mzee
WANANCHI WANAOMFAHAMU NIHIFADHI
Mussa Juma amesema mwanamke huyo ni mfano wa kuingwa kwani hajawahi kukata tamaa katika maisha yake kwasababu hajachoka kupambana ikiwa kwenye siasa pamoja na shughuli mbalimbali za kijamii. “Nihifadhi ni mfano wa kuingwa kwasababu kwanza ni mchapa kazi, mwanake asiekubali kushindwa, anaejiamini na yupo tayari kwa mapambano mda wote hajawi kukata tamaa japo kuwa wapo wanaotamani asishiriki katika nafasi yoyote kwani ameanza kuwaogopesha.”Musaa
Huku baadhi ya wanawake wenziwe wanatamani kuwa kama nihifadhi lakini anashindwa kutokana na woga aliokuwa nao wa kushiriki katika siasa.” Napenda niwe kama nihifadhi, lakini siku zote itakuwa ndoto tu ya kutamani kuwa kama yeye kwasababu naogopa kushiriki katika nafasi za uongozi, na woga wangu unakuja pale wakati washindana na mwanaume, ukiachia ilo rushwa ya ngono ninayoisikia nazidi ndio nazidi kuakata tamaa kshiriki nafasi za uongozi.”Amesema Mgeni
0 Comments