Na Ahmed Abdulla na Amrat Kombo
Jumla ya
kazi za waandishi wa habari 161 zinazotoa ushawishi juu ya upatikanaji wa
sheria mpya ya habari Visiwani Zanzibar zimeandikwa na kurushwa katika vyombo vya
habari tofauti ikiwemo radio, televisheni,mitandao ya kijamii  na magazeti kwa kipindi cha mwaka mmoja
kutoka mwejzi Julai 2023 hadi Juni 2024.
Akiwasilisha
mrejesho wa kazi kwa niaba ya afisa  ufatiliaji
na tathimini Khairat Haji alisema hiyo ni baada ya waandishi wa habari 25  kutoka Unguja na Pemba kupatiwa mafunzo ya na
namna bora ya kufanya ushawishi kwenye taarifa zao wanazoziandika kwa lengo la
kupata sheria Mpya ya habari itakayopanua uhuru wa waandishi wa habari na
vyombo vya habari.
alisema mrejesho
huo unaonesha kuwa waandishi 15  kutoka Unguja
walipatiwa elimu hiyo na chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania Upande
wa Zanzibar TAMWA-ZNZ ni waandishi wa habari 10 tu ndio  walifanikiwa 
kutoa mrejesho  wa kazi
walizofanya  ambazo ziliweza kutoa maoni
tofauti katika vichwa vya watu.
Afisa
mratibu wa sheria za habari Zaina Mzee alisema ikiwa ni mwaka  wa pili sasa katika kuhamasisha upatikanaji
wa sheria mpya ya habari lakini sheria hiyo haijapatikana licha mwanga kuanza
kuonekana.
“Tulishakutana
na viongozi mbalimbali  kujadili jambo
hili kwa jumla ni mikutano mitano ambayo ilifanywa na wadau wa habari  (ZAMECO) wakiwa na tume ya kurekebisha sheria
,tume ya utangazaji, viongozi wa baraza la wawakilishi na viongozi wengine lakini
bado halijapata muwafaka” alisema Zaina.
Aidha
alisema sheria ya habari iliyo rafiki pekee ndio inayoweza kuiheshimisha tasnia
ya habari hivyo  wadau wa habari wanatakiwa
kuongeza nguvu ya ushawishi wa upatikanaji wa sheria mpya na rafiki ya habari
ili kuona inajitengemea na haingiliwi na mamlaka yoyote kwani kinyume na  hivyo kunakosesha uhuru wa kujieleza na kutoa
taarifa.
Mjumbe wa
bodi wa chama cha waandishi wa habari 
wanawake Tanzania Upande wa Zanzibar TAMWA-ZNZ Hawra Shamte aliwataka
waandishi kuendelea  kutumia kalamu zao
kuhakikisha sheria ya habari  rafiki
inapatikana 
Bi Hawra
aliendelea kusisitiza kuwa “tunategemea sheria zetu zitatoka kwa makatibu wakuu
na kuacha kupigwa dana dana kutokana na ahadi tunazopewa kwa sheria zetu kuu
mbili za habari ikiwa ni wakala wa usajili magazeti, na tume ya utangazaji kwa
sababu tushazisemea sana na tunazidi kuziandikia  hadi tuone mafanikio”
Kwa upande
wake muandishi wa habari mkongwe Salim Said Salim aliwaomba waandishi  kutokata tamaa  na kuendelea 
kuandika na kusemezea sheria hizo mpaka kufikia malengo.
Pia alisema “Tunatakiwa
kuandikia stori au makala zitakazoonesha 
mifano ya nchi waliofanikiwa kuwa na sheria a habari rafiki kama Kenya  na Uganda ili kuleta hamasa zaidi ya kupatiwa
sheria mpya”.
Nao baadhi
ya mwaandishi  waliopatiwa mafunzo hayo walisema
wataendele kuandika habari zinazohusu mapungufu ya sheria za sasa za habari
kwasababu lengo halijatimia kwani waandishi wa habari ni  moja ya wahanga wa mkandamizo wa sheria hizo
“Tukipata
sheria rafiki itakuwa rahisi kwetu kupata taarifa bila vikwazo” walieleza
 


 
 
 
0 Comments