Na Ahmed Abdulla, Zanzibar:
Ikiwa ni takriban
miaka 20 sasa wadau wa sekta ya habari wakipaza sauti juu ya uwepo wa sheria za
habari ambazo zinakandamiza uhuru wa waandishi wa habari na vyombo vya habari.
Miaka yote hiyo
bado hakujapatikana muafaka kutoka kwa serikali juu ya upatikanaji wa sheria
mpya jambo lanaloendelea kudumaza ufanisi wa vyombo vya habari kwani hakuna
uhuru wa moja kwa moja kwa vyombo hivyo.
Miongoni mwa
sheria hizo ni ile Sheria ya Usajili wa Wakala wa Habari, Magazeti na Vitabu Na.
5 ya mwaka 1988 na Sheria ya Tume ya Utangazaji Na. 7 ya mwaka 1997.
Miongoni mwa vifungu vyenye utata katika Sheria ya Usajili wa Wakala wa
Habari, Magazeti na Vitabu Na. 5 ya mwaka 1988 kifungu cha 27 (1) ni pale
inapompa mamlaka Afisa wowote wa jeshi la polisi kukamata gazeti lolote, popote
linapopatikana ambalo limechapishwa au anashuku limechapishwa habari kinyume na
sheria hii.
Dkt. Mzuri Issa ni
Mkurugenzi wa chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania Upande wa
Zanzibar TAMWA-ZNZ alizisisitiza mamlaka zinazohusika na marekebisho ya Sheria kuharakisha
mchakato wa sheria za habari ili kupatikana kwensheria mpya za habari
zinandolinda uhuru wa habari.
“Endapo itapatikana sheria
inayotoa uhuru wa habari itaisaidia serikali kupiga hatua za maendeleo kwani
waandishi wataandika habari zinazogusa uwajibikaji lakini pia wananchi
watanufaika kupata habari zenye uzito zenye kuibua mambo mbalimbali yenye tija
kwa taifa” alisema Dkt. Mzuri
Mwandishi kutoka kwa Mtandao
wa The Chanzo Najat Omar amesema kuwepo jwa sheria ambazo si rafiki wa
waandishi wa habari kunaweza kuchochea ufisadi katika taifa kwani waandishi
watakuwa na hofu ya kuandika habari hizo kwa kuhofia usalama wao.
“Athari kubwa zaidi ni
kutokuwa na taarifa sahihi sababu waandishi wataandika habari za kupongeza
zaidi na kushukuru tu” alisema
Kwa upande wa Mwandishi wa
habari mkongwe visiwani Zanzibar Salim Said alisisitiza kwamba vyombo vya
habari havina nia mbaya kwa Serikali bali ni washirika muhimu katika kuleta maendeleo
kwa jamii huku akisema kuwa upatikanaji wa sheria inayotoa uhuru kwa vyombo vya
habari ni muhimu.
Je kwa miaka hiyo serikali
imefikia wapi juu ya marekebisho ya habari hizo?
Mnamo May 03, 2023 katika maadhimisho ya siku
ya uhuru wa Vyombo vya habari diniani Rais Dk. Mwinyi, alizungumzia mchakato wa
marekebisho ya sheria ya Habari, ambapo alisema Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar tayari imeandaa mswada wa sheria hiyo yenye madhumuni ya kufuta
Sheria iliyopo ya Usajili wa Magazeti, Wakala wa Habari na vitabu Sheiria
nambari 5 ya mwaka 1988 ambapo marekebisho yake ni sheria nambari 8 ya mwaka
1997 na kutunga Sheria mpya ya Huduma za Habari na Mambo yanayohusiana na hayo.
Dk. Mwinyi alieleza kwamba Mswada huo tayari uko Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu na unatarajiwa kutoa sheria nzuri itakayohusiana na masuala ya
habari.
Lakini hayo yakiendelea
lakini hadi leo mswaada huo haujajuulikana ni lini utakuwa sheria rasmi.
Hivyo ni jambo la kufurahisha
kuona kila mmoja kwa nafasi yake anatekeleza wajibu wake ili kuona mswaada huo
unakuwa sheria.
0 Comments