Ticker

6/recent/ticker-posts

Kwanini Nafasi Za Uongozi Kwa Watoto wa Kike Maskulini Ni Kidogo?

 


Na Amrat Kombo, Zanzibar:

Uongozi ni wajibu kwa kila mtu ikiwa mwanaume au mwanamke hata kundi la watoto wakiwa wakike au wakiume wanaweza kuwa viongozi kwa aina yao na sehemu waliyo ndani ya jamii zao.

Lakini wanaume warika mbalimbali  wamekuwa ndio waongozaji katika sekta mbalimbali kuliko wanawake, na hii kutokana na  mtazamo finyu wa jamii kuona mwanaume ndio anaepaswa kuwa kiongozi .

Uongozi nini ?

Uwongozi ni mamlaka ya kuwaonyesha watu njia kwa vitendo.

Vilevile uongozi ni jinsi gani kiongozi anaweza kuleta ushawishi kwa watu na kufikia maendeleo yaliyotarajiwa.

Kuna aina  njia nyingi za kuainisha uongozi lakini njia ya msingi ni kuangalia jinsi kiongozi alivyoingia madarakani na utaratibu wake wa kuongoza.

Katika viongozi wapo Wafalme, Maraisi, Mawaziri, Watemi, Machifu, Wakurugenzi, Viongozi wa dini.

Viongozi wanawake ni wachache katika sehemu mbalimbali ikiwemo mashuleni hadi katika tasisi mbalimbali. Nahii kutokana na mfumo dume uliowekwa tangu enzi za ukoloni.

Hali hii inawafanya wanawake wengi kukosa elimu,urithi, nafasi za uwongozi   na kuwa na sauti iliyosikika na kuheshimika katika kufanya maamuzi.

Raisi Mstaafu wa Skuli ya Bembelela Zanzibar Lelam Abdallah Twaha alisema sababu zinazopelekea wanaume kuwa wengi katika sehemu ya uwongozi katika kazi tofauti ikiwemo ya  maskulini.

" Wanaume kutotaka kuongonzwa na wanawake,vilevile wanawake kuogopa kujitokeza katika nafasi za kugombea, baadhi ya walimu kupenda mwanaume ndio awe kiongozi."

Sambamba na hayo amesema faida mbalimbali amepata wakati alipokuwa kiongozi wa skuli hiyo ikiwemo kujiona mzalendo,kuongeza ujuzi,kujiamini katika sehemu yoyote .

Mwanafunzi wa Skuli hiyo Hunaida Haji Juma alisema kuna tofauti mbalimbali za kuongoza kwa mwanaume na mwanamke.

" Mwanamke anazidi kukemea suala la udhalilishaji tofauti na mwanaume,vilevile mwanamke anatoa nafasi za uwongozi  mbalimbali kwa wanawake wenzake tofauti na mwanaume .

Sambamba na hayo amesema kuna idadi ndogo ya viongozi wanawake maskulini hasa katika nafasi za uraisi.

" Takribani ya skuli nyingi maraisi wanaume baadhi ya skuli ndio utakuta raisi mwanamke ikiwemo skuli ya faraja, bembela na alhisani na skuli hizi mbili kwakuwa hawana wanaume ndio ilapelekea wanawake kuwa raisi." alisema hunaida

 Mwanafunzi wa Skuli ya Lumumba Imraan Iddi Hamadi alisema nafasi za uwongozi ni chache kuanzia ngazi za skuli hadi katika tasisi nyengine kutokana na kuwepo kwa mfumo dume,usawa wa kijinsia,pamoja na wanawake kutokuwa na muamko wa kuweza kuongoza.

" Kuna sababu nyingi ambazo zinawafanya wanawake kuwa nyuma katika nafasi za uwongozi ikiwemo kutokuwepo kwa usawa wa kijinsia kwasababu nafasi nyingi wanapewa wanaume za uwongozi kuliko wanawake nahii inatokana na kuona kuwa wanawake hawawezi kuongea au kujituma." alisema

Mwanafunzi wa Skuli ya  Lumumba  Salima Shamimu khamis amesema kuna faida mbalimbali ambazo zinapatikana endapo mwanamke akiwa kiongozi ikiwemo kutakuwepo na usawa wa kijinsia,mwanamke kuchanganua vitu mbalimbali pamoja na kufanya ubunifu kwa lengo la kuinua uchumi wa nchi.

Pia  amewaaasa wanafunzi wenziwe kuchangamkia fursa katika nafasi mbalimbali za uwongozi katika skuli itamsaidia kupiga hatua hadi kufikia nafasi za juu za uwongozi.

 Mwalimu wa Skuli ya Sekondari Bembela  Abdallah kombo khamisi amethibitisha kuwa kuna sababu nyingi ambazo zinawanyima nafasi za uwongozi wanawake .

" Wanaume wengi wamepata taaluma ya uwongozi kuliko wanawake,wanaume wanajiamini  mbele za watu kuliko wanawake ,pamoja na baadhi ya watu kuwa na itikadi za kidini kuwa mwanamke hawezi kuwa kiongozi." alisemaPia amesema licha ya kuwepo kwa mitazamo hiyo kwa watu lakini wanawake wameeanza kuchangamikia fursa hiyo kwa kupata taaaluma za uwongozi kuanzia nganzi ya nchini hasa mashuleni hadi nafasi za juu.

Aidha amesema ili kuwepo kwa idadi nyingi ya viongozi wanamke inahitajika kupewa elimu katika sehemu mbalimbali ikiwemo mashuleni hadi katika shughuli mbalimbali za kijamii.

" kila mtu anahaki ya kuongoza na ili mwanamke aweze kupata nafasi katika uwongozi waanze kupewa elimu tangu wakiwa skuli za msingi kwa lengo la kumjenga na kweza kujiamini hii itamsaidia kwa  kupenda kuongoza hadi kufikia nafasi za juu bila ya uwoga.

Post a Comment

0 Comments