Ticker

6/recent/ticker-posts

Elimu Ya Matumizi Ya Mitandao Ya Kijamii Kwa Wanasiasa Wanawake

 


Na Ahmed Abdulla, Zanzibar:

Hii ni karne ya 21ambayo Kasi ya technolijia inazidi kuimarika duniani.

 

Zanzibar nayo ni sehemu ya dunia ambayo matumizi ya teknolojia hiyo yamekuwa kwa kasi.

 

Mitandao ya kijamii ni sehemu ya teknolojia hiyo ambayo kwa Takwimu kutoka Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) hadi kufikia mwezi Disemba 2023 watanzania 34,469,022 kati ya 61,741,120 wa wanatumia huduma za intaneti hiyo ikiwa na maana wanatumia mitandao ya kijamii.

 

Zanzibar ikiwa ni miongoni mwa nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania watu wake hawako nyuma katika matumizi ya mitandao ya kijamii lakini jee wanawake wanaitumia mitandao hiyo kwenye kusaka uongozi?

 

Suhaila Ussi Pondeza ni mjumbe wa kamati ya utekelezaji Umoja wa wanawake wa chama cha Mapinduzi Tanzania (UWT) wilaya ya Amani Kichama alisema licha ya kuwa na Kurasa za mitandao ya kijamii lakini hatumii kwenye harakati zake za kisiasa.

 

“Sasa naanza kushawishika kwenye kutumia mitandao ya kijamii kwenye harakati zangu za kisiasa maana naweza kuwafikia watu wengi kwa muda mfupi” alisema Suhaila

 

Maua Mohammed Mussa ni mwanasiasa mwanamke ambaye Mwaka 2020 aligombea nafasi ya Ubunge jimbo la Shaurimoyo kwa tiketi ya Chama Cha ACT-Wazalendo alisema hakutumia mitandao ya kijamii kwenye harakati zake za kuwania nafasi hiyo huku akiitaje elimu ya matumizi ya mitandao hiyo ndio ilikuwa changamoto kwake.

 

“Nafahamu kwamba nilikosa mengi kwa kukosa kwangu kutumia mitandao ya kijamii likini tatizo kubwa ni kuwa wanawake wengi tuna changamoto ya kutokuwa na elimu juu ya matumizi ya mitandao hiyo” Alisema

 

Kwa upande wa katibu wa Umoja wa Wanawake Wa Chama cha Mapinduzi Tanzania (UWT) wilaya ya Kati alisema wanatambua kuwa wanasiasa wanawake wa chama hicho bado hawana muamko wa kutumia mitandao ya kijamii kwenye masuala ya siasa ilhali ndio sehemu yenye kundi la watu wengi.

 

“Tunachokifanya kwa sasa ni kuwashawishi wanawake watumie mitandao ya kijamii kwani kuna fursa kubwa ya kujitangaza” Alisema

 

Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano kutoka chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Upande wa Zanzibar (TAMWA-Zanzibar)Sofia Ngalapi alisema TAMWA imebaini kuwa wanasisa wengi wanawake wanazo kurasa za mitandao ya Kijamii lakini wanashindwa kuitumia fursa iliyopo huko kwa ajili ya kufanikisha malengo yao.

 

“Wengi wao wanazo kurasa za mitandao ya kijamii lakini hawazitumii kwenye harakati zao za siasa ila wajuwe wanakosa fursa ya kujitangaza kwa watu wengi ndani ya muda mfupi” Alisema

 

Pia aliwasisitiza wanasiasa wanawake na vijana kuitumia mitandao ya kijamii katika kubadilishana mawazo na wanasiasa wabobezi wanaotumia mitandao hiyo.

 

Kwa muktadha huo inaonyesha kuwa Licha ya fursa nyingi zilizopo kwenye mitandao ya kijamii lakini bado wanasiasa wanawake wako  kwenye usingizi mzito juu ya matumizi ya mitandao hiyo.

 

Ni jambo jema sasa kwa kila mwanasiasa mwanamke kuanza kutumia mitandao ya kijamii kwenye harakati za siasa ili kuona wanafika kule ambako wanaharakati wa kupigania usawa wa kijinsia kwenye uongozi na demokrasia hasa kwa kuzingatia ni mwaka mmoja tu umesalia kabla ya kufika kwa uchaguzi mkuu wa dola visiwani Zanzibar.

 

Post a Comment

0 Comments