Na Thuwaiba habibu:
Mratibu wa wanawake na watoto wa shehiya ya Bumbwini makoba shida Issa Rashid amewataka wanawake wenzake kujitokeza kwa wingi katika kugombania nafasi za uongozi wakati zikitokea.
Ameyasema hayo wakati alipokuwa katika darasa la watu wazima huko bumbwini mkoa wa kaskazini B" Unguja alisema nimeamua kuanzisha darasa hili kwani nimeona ipo haja ya kila mwanamke kupata elimu ili awaze kuelewa vitu kwa urahisi na kuwapunguzia uoga wanapotaka kugombea nafasi hizo.
‘’Nimefanya hivyo ili kila mtu aweze kupata fursa ya elimu kwani ni muhimu kwa kila mtu kwa vile pia itawawezesha wanawake kuweza kuchukua nafasi za kuongozi’’
Kwa mtazamo huo wanawake wana kila kigezo cha kuwa viongozi wazuri na elimu itawasaidia mwanamke kujiamini na kuwa na uwezo na ujasiri wa kugombea uongozi kwa vile siku zote huwa karibu na jamii na kulewa vyema matatizo yaliopo.
Aidha alisema lengo la kuanzisha elimu ya watu wazima katika kijiji chao ni kutaka kila mtu anaweza kujuwa kusoma na kuandika na kuhesabu.
Mafunzo aliyoyatoa yamesaidia watu wengi waliokosa bahati ya kupata elimu walipokuwa wadogo kuweza kusoma na kuandika kwani hapo nyuma hawakuweza kuwa viongozi,lakini kwa sasa kumeweza kusikika hata sauti zao kwa mambo yanayowahusu katika maisha yao ya kila
Nae mmoja wa hao wanafunzi wa darasa la watu wazima , Bi. Navuli Ameir, alisema alishindwa kusome alipokuwa mdogo kutokana na hali duni ya kimaisha katika familia yake..
Lakini baada ya kuwaona wenzake wanakwenda kudoma aliamuwa kuomba wazee wake wampeleke ili ilikuwa ni ngumu kwa wakati huo .
‘’Niliona wenzangu wakitoka madrasa ya Quran wanaelekea skuli ila kujipatia elimu. Lakini mimi nilipotaka nipelekwe skuli niliambiwa hapakuwepo uwezo’’, alielezea
Alisemailiumia sana, lakini hakuwa na la kufanya ili naye aweze kwenda skuli kama watoto wenzake. na aliiambia nafsi yake kuwa ikitokea fursa ya kupata elimu hataiachia ipotee na alishukuru kwamba nafasi hio ilikuja kwa kufunguliwa darasa la elimu ya watu wazima.
Pia alisema sasa akipata barua anaweza kuisoma na anaweza kuelewa ujumbe uliopo kwenye maandishi.alisema wanajitahidi kushirikiana na wanawake kuleta maendeleo katika kijiji chao na kuanzishwa kwa masomo ya elimu ya watu wazima ni fursa nzuri ya
Kwa upande wake mjumbe wa sheha Othamani Ussi machano alisema wanajitahidi kushirikiana na wanawake kuleta maendeleo katika kijiji chao na kuanzishwa kwa masomo ya elimu ya watu wazima ni fursa nzuri ya kuwakomboa akina mama
Alisema siku hizi wanawake wamekuwa na muamko mkubwa wa kushika nafsi za uongozi
Hii ni hatua nzuri ya wanaume na wanawake kwenda sambamba katika kujitafutia maendeleokatika shehiya yao.
0 Comments