Mwaakilishi Jimbo la Tunguu Simai Mohamed Said amekabidhi seti 32 za Jezzy pamoja mipira hamsini kwa vilabu 30 vilivyomo ndani ya jimbo hilo.
Simai amesema hatua ya kukabidhi vifaa hivyo ni katika jitihada za kuinua sekta ya michezo kwa vijana jimboni na kuufanya mchezo wa mpira miguu kuwa sehemu ya ajira kwa vijana hao.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Jimbo la Tunguu Mtumwa Ali amepongeza juhudi hizo huku akiwataka vilabu vilivyopatiwa vifaa hivyo kuvitumia vizuri na kueleza kwa jamii juu ya utekelezaji wa ilani ya CCM ili wananchi waendelee kukiamini chama hicho.
Nao baadhi ya viongozi wa vilabu hivyo wamesema awali walikua wanakabiliwa na changamoto ya vifaa ikiwemo mipira na jezzy hivyo kutolewa kwa vifaa hivyo na mwakilishi kunaondosha changamoto hiyo
0 Comments