Ticker

6/recent/ticker-posts

Iko Wap Nafasi Ya Mwanamke Mwenye Ulema Kwenye Uongozi Ndani ya Vyama vya siasa?

Na Ahmed Abdulla, Zanzibar:


Wanawake wenye ulemavu wanamchango mkubwa katika kuleta maendeleo ya taifa  na nafasi katika kukuza demokrasia nchini.

Maendeleo hayo si kwamba yatamfaa Mwenye ulemavu pekee bali hata asiyekuwa na Ulemavu.

Katika uchaguzi wa mwaka 2020 Zanzibar iliandikisha wapiga kura 566,352 lakini waliopiga kura ni watu 498,786.

Katika watu hao waliopiga kura watu wenye ulemavu walikuwa ni 4680 ambao wanawake kati yao ni 2197 na wanaume ni 2483.

Lakini kwa upande wa wagombea wanawake wenye ulemavu kwa nafasi mbalimbali kuanzia wadi hadi Taifa kulikuwa na wagombea mgombea mmoja tu na ilikuwa ni nafasi ya Udiwani.

Hii inatokana na vyama vya siasa kutokuwa na utamaduni wa kuibua vipaji vya viongozi wanawake wenye ulemavu kwani hata hao wachache walioomba ridhaa ya kugombea sehemu Fulani hawakuteuliwa na vyama vyao.

Tunu Juma Kondo ni Naibu Katibu Mkuu Umoja wa wanawake Tanzani upande wa Zanzibar, Chama Cha Mapinduzi (UWT) amesema bado wanawake wenye Ulemavu wamemekuwa waoge kwenye kugombania wadi, majimbo na Uraisi.

“Tumeweka nafasi maalum za watu wenye ulemavu kwenye uwakilishi na ubunge kwani tunaona bado wana uoga wa kenda majimboni na kwenye wadi”

Bi. Tunu pia amewasisitiza wanawake wenye ulemavu kuondoa hofu pale wanapohitaji kugombea sehemu yeyeote.

Jamila Borafia Hamza ni mwanamke wenye ulemavu wa uoni, aliwahi kugombea nafasi ya uwakilishi katika jimbo la Mwanakwerekwe kuptia Chama Cha Mapinduzi, hakufanikiwa kinyanganyiro hicho aliishia chaguzi za ndani ya jimbo.

Alisema moja ya changamoto aliyokutana nayo ni kukosa usafiri wa uhakika kuwafuata wajumbe kwa ajili ya kunadi sera zake.

“kama Tunavyotambua wajumbe hawaka katika eneo moja na mtu mwenye ulemavu hawezi kwenda peke yake, kwa hiyo kumfuata mjumbe mmoja baada ya mwengine ni kipengele na wengi wetu tunashindwa hapo” Alisema Jamila

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Chama Cha Ada Tadea Juma Ali Khatib alisema chama chao kinawapa nafasi kubwa wanawake wenye ulemavu wanapojitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.

“tulikuwa naye mgombea mmoja mwanamke mwenye ulemavu na aligombea ubunge wa Kikwajuni, tulimsaidia mambo mbalimbali hata kumbeba kumuweka kwenye jukwaa ili aombe kura” Alisema Juma Ali Khatib

Kauli ya serikali ni ipi juu ya wanawake wenye uongozi wenye nia ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi?

Katibu Mtendaji wa baraza la watu wenye ulemavu, ofisi ya makamu wa kwanza wa Raisi Zanzibar Ussi Khamis Debe alisema ofisi inatajia kukutana na vyama vya siasa kwa lengo la kuwawekea mazingira wezeshi wanawake wenye ulemavu ili wafanikishe azma zao bila uwepo wa changamoto zinazosababishwa na ulemavu wao.

“kubwa linalokuja ni kuweka mazingira wezeshi ya Kampeni, kwamba majukwaa yaendene na hali za watu wenye ulemavu husika” alisisitiza

Ni dhahiri kuwa bado wanawake wenye ulemavu hawajawa na muamko mkubwa kwenye kugombea nafasi za uogozi katika wadi, majimbo na hata uraisi.

Hivyo ni budi kwao kujitokeza kwa wingi kwenye vinyanganyiro vya nafasi hizo na vyama vya siasa viwaunge mkono kwa asilimia mia kwenye mchakato wao wa uchaguzi

Post a Comment

0 Comments