Ticker

6/recent/ticker-posts

Waumini Wa Kiislam Wahimizwa Kutekeleza Ibada Ya Umrah


Na Kazija Thabit Zanzibar. 

WAUMINI wa Kislamu wametakiwa kuharakisha kuwahi muda uliobakia kwa ajili ya kwenda kujisajili ili kuwahi ibada ya Umra kabla ya February 25.


Kauli hiyo imetolewa na Tasisi ya Furqan Hajji and Umra ambayo Leo imeanza safari na msafara watu 16  wakiwemo viongozi wawili kuelekea Makka Saudi Arabia kwa ajili ya ibada ya Umra. 


Akizungumza kabla ya kuondoka katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa ABEID Amaan Karume, Zanzibar Abubakar Khudhaifa Ahmad kutoka Taasisi ya Alfurqan Hajji and Umra alisema ibada hiyo ni muhimu kwa muislamu mwenye uwezo kwani inasaidia kujifunza mengi ya dini ya kiislamu. 


Alisema  kwa mujibu wa maandiko katika vitabu vya dini ya kiislamu vinaeleza kuwa ibada hiyo huondoa ufakiri, hutatua matatizo tafauti, hivyo aliwataka waumini  kuachana na mambo ya kuwategemea waganga Bali wamtegemee Mungu kwa kufanya ibada kama umra. 


Alifahamisha kuwa Taasisi yao inasajaili waumini kwa hiyo wanaotaka kwenda kufanya ibada hiyo wa wahi   mapema kwa ajili ya kuanza utaratibu wa kujisajili na kuanza  ibada hiyo kwani Hijja na Umra ni  nguzo ya 5 kiisalam. 


Pia aliwahimiza waamuni kujisajili kabla muda haujaisha ambapo  mwisho February 25  kwa mwaka huu hivyo wanaohitaji na wenye uwezo wa wahi mapema katika Taasisi zilosajiliwa za uhakika. 


Alisema ibada hiyo inawahistakihia wale wenye kumiliki milioni 16 au wenye uwezo wa vitu vya ziada ikiwemo nyumba 2 au Gari yenye thamani ya milion 20 hivyo sio lazima uwe mamilioni ya mapesa. 


Mbali na hayo alisema wataungana na mautamirina waliopo Dar res  Salam ambapo watanza safari kuelekea Oman na badae Jidda na badae kuelekea Mji  Mtukufu wa Makka ambapo watakaa siku 5 kwa ajili ya ibada na kuangalia sehemu za historia. 


Alisema pia Wataenda Madina na kukaa  siku 5 ambapo madina Kuna sehemu nyingi za ibada na historia hivyo pia watapata kuzingalia ambapo jumla ya masiku 10 ndiyo watakua katika ziara hiyo ya safari ya Umra  na badae watarudi Tanzanian Lakini pia safari nyengine inatarajiwa kufanyika Ramadhani. 

Post a Comment

0 Comments