Mahakama ya Mkoa wa Kaskazini Unguja imemuhukumu mshtakiwa Abdi Khamis Mselem mwenye umri wa miaka 20 mkaazi wa mahonda kutumikia kifungu cha miaka 14 chuo cha mafunzo na kulipia fidia ya shilingi milioni moja .
Awali ilidaiwa kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa la kulawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 11 mnamo tarehe 6/3/2023 kinyume na kifungu namba 115(1) na kosa la kutorosha kinyume na kifungu namba 113(1)(b) vya sheria namba 6/2018.
Kesi hiyo ilifunguliwa mahakamani tarehe 24/4/2023 na jumla ya mashahidi sita walitoa ushahidi wao mahakamani na kusoma hukumu hiyo leo.
Akisoma hukumu hiyo hakimu wa mahakama Luciano Makoye Nyengo amesema mahakama imejiridhisha na ushahidi uliotolewa mahakamani ambao hauna chembe ya shaka ndani yake na kumtia hatiani mshtakiwa kwa makosa hayo .
0 Comments