Ticker

6/recent/ticker-posts

Afya Ya Akili Ipewe Kipaumbele: Riziki Pemba

 

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Riziki Pembe Juma, Akizungumza katika  bonanza la kuadhimisha kuelekea siku ya afya ya akili na maafa duniani lilofanyika katika jengo la Chuo cha Afya Zanzibar Wilaya ya Magharib “B” Unguja, Oktoba 9,2023

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Riziki Pembe Juma amewataka wananchi kuzingatia umuhimu wa Afya ya akili ili kuzuia maafa ambayo yanayoweza kutokea na kupelekea athari kubwa kwa katika mwili wa binadamu.

Akizungumza katika  bonanza la kuadhimisha kuelekea siku ya afya ya akili na maafa duniani lilofanyika katika jengo la Chuo cha Afya Zanzibar Wilaya ya Magharib “B” Unguja, amesema  kila mwananchi anapaswa kutambua umuhimu wa afya ya akili kama ilivyo afya ya mwili ili kujikinga na maafaa ambayo yanawezakujitokeza.

Amesema afya ya akili ni muhimu kwa kila mtu kwani inamuwezesha kuishi maisha yenye furaha, tija na kujisikia vizuri ulimwenguni. Lakini mara nyingi suala hili halipewi kipaumbele kinachostahili.  Hivyo Waziri huyo  amehimiza suala la afya ya akili kupewa kipaumbele na kila mtu, kutambua kwamba  ni sehemu muhimu ya afya kwa ujumla.

“Afya ya Akili ni muhimu kwa kila mmoja wetu, kwani maafa hayachagui  mtu wa kumuathiri, yanaweza kumuathiri mtu yeyote, mahali popote, wakati wowote” Alisema Waziri Pembe.

 

Alifahamisha kwamba kila ifikapo tarehe 13 Oktoba, huadhimishwa Siku ya Afya ya akili na maafa Duniani, siku hii inawakumbusha watu/jamii juu ya umuhimu wa kuwa tayari katika kukabiliana na maafa yanayoweza kutokea.  Pia alisema siku  hiyo huongeza uelewa wa afya ya akili na kuleta mabadiliko chanya kwa afya ya akili ya kila mtu.

 

Aidha Waziri Pembe alisema mwaka huu 2023, katika kuadhimisha Kimataifa siku ya Afya ya akili itachunguza uhusiano wa pande mbili kati ya maafa na usawa wa kijinsia, hivyo amewaomba wananchi kupenda  kukuhimizana kushiriki katika kila tukio la kuendeleza umoja, au kujiunga na mazungumzo juu ya kupambana na usawa wa kijinsia  kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu.

 


Mapema Mkurugenzi Mtendaji Chuo cha Afya Zanzibar (ZSH) Aziza Hemed ametoa wito kwa wananchi kuwa mabalozi wazuri kuhamisha jamii kupata ushauri nasihi na kisaikolojia pale ambapo wanapopata matatizo za kimaisha kwani hatua hiyo inaweza kupunguza athari za maafa ambazo zinatokana na binadamu.

 

Kupitia bonanza hilo shughuli mbali mbali zimeandaliwa ikiwemo debeti,michezo,utowaji wa zawadi pamoja na zoezi la kuhitimisha program ya mafunzo ya msingi “Crash Program”.

 

Post a Comment

0 Comments