Na Ahmed Abdulla:
ZAIDI ya wakulima 21,000 wanatarajiwa
kunufaika na mradi wa viungo chini ya usimamizi wa Agri-connect ambapo unalenga
kuwaelimisha wakulima ili kuongeza uzalishaji katika maeneo Yao na kumfanya
mkulima aweze kulima kilimo Cha biashara na kujikwamua na umasikini.
Katika wakulima
hao 21,000 watakaonufaika na mradi huo watu zaidi ya 16,000 wameshaanza
kunufaika hadi inayoifanya idadi hiyo kukaribia nusu na robo ya malengo.
Wakati wakulima
hao zaidi ya 16,000 wakiendelea kupatiwa mafunzo na nyenzo mbalimbali jee
maendeleo ya kilimo chao yakoje na jee yameanza kubadilisha hali za maisha yao.
Vua Ali Songoro
ni mkulima ambaye amenufaika na mradi wa viungo ambapo amesema mradi huo umempa
manufaa makubwa kutoka kilimo cha mazoea na sasa kulima kilimo chenye tija.
“nilikuwa
nimekaa nyumbani kama mkulima wa kawaida lakini baada ya Mradi huu kupitia kwa
Chama cha Waandishi habari wanawake TAMWA-ZNZ walinishauri tusaidiane kwenye
kilimo nikakubali na sasa najivunia kilimo ndio kinaniendeshea maisha yangu”
alisema mkulima huyo
Mradi wa
kilimo haukujikita tu kwenye wakulima bali hata wasarifu bidhaa za kilimo ambapo
mwandishi wa habari hizi alikutana na Saida Mohammed Shaib anayejishugulisha na
usindikaji wa bidhaa ambapo alisema mafunzo ya mara kwa mara juu ya shughuli
zake yamemjenga kuwa na ujasiri wa kupambana licha ya kukabiliwa na changamoto
mbalimbali ikiwemo kutokueleweka katika jamii ambapo sasa ameondoka kwenye
utegemezi.
“mafanikio
yanaonekana kwasababu kabla kila kitu nilimtegemea baba yangu lakini sasa
namudu kuendesha maisha yangu” alisema Saida
Ali Said
Juma ni msimamizi wa mkuu kwa wakulima
Kupitia alisema wakulima waliowafikia ni
wale wamekuwa na kasi ya uzalishaji sambamba na kuwa na uhakika wa masoko.
“tulichogundua
ni kuwa wakulima wanaomiliki miundombinu ya maji au tuliowasaidia miundombinu
ya maji ni wakulima ambao wana uwezo wa kuzalisha kwa uharaka na uzalishaji wao
ni mkubwa na wana masoko ya uhakika”
Alisema msimamizi
huyo
Mtaalamu wa
kuendeleza sekta ya kilimo Dk Anasia Gasper Maleko yeye alisema ongezeko la uzalishaji wa bidhaa za mbogamboga viungo na
matunda ni miongoni mwa mafanikio
yaliyopatikana katika mradi huo Jambo ambalo linapelekea wakulima wadogowadogo kunufaika
katika sekta hiyo.
Alisema
mradi huo umekuja kuongeza nguvu kwa wakulima wadogowadogo ili kuongeza mnyororo
wa Thamani katika uzalishaji hivyo aliwataka wakulima hao kuzidi kufuata
utaratibu wa wataalamu wa kilimo kwa maendeleo zaidi.
Mradi wa
mboga mboga viungo na matunda unatekelezwa na chama Cha wandishi wa habari
Wanawake TAMWA Zanzibar,Community Forest Pemba na PDF kuwa kushirikiana na
jumuia za Ulaya ili kuweza kufanikisha malengo ya wakulima wadogo wadogo katika
kuimarisha mnyororo wa Thamani katika kilimo chao
0 Comments