Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu. HEMED SULEIMAN ABDALLA akishiriki ujenzi wa Soko dogo Chuwini |
MJUMBE wa
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa amewataka Viongozi na
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kuhakikisha vijana waliotimiza umri wa miaka
18 wanajiandikisha ili kupata kitambulisho cha Mzanzibari mkaazi pamoja
na kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili kuweza kukichagua
na kukipa ushindi chama hicho ifikapo uchaguzi mkuu wa nchi mwaka 2025.
Mhe.
Hemed ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameyasema hayo wakati
akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na wananchi katika
ziara yake ya kukagua uhai wa Chama katika Jimbo la Mfenesini,Jimbo la Mwera
pamoja na Jimbo la Welezo Wilaya ya Mfenesini Kichama.
Amesema
Viongozi wa ngazi mbali mbali katika majimbo hayo ndio kiunganishi kizuri
ambacho kitaweza kukivusha chama Cha Mapinduzi ifikapo uchaguzi mkuu wa nchi
hivyo ni lazima kuhakikisha wanawasimamia ipasavyo wanachama wa chama hicho
pamoja na kuhakikisha wanaongeza wanachama wapya wenye kukiletea ushindi chama
cha mapinduzi.
Amesema
Viongozi wanajukumu la kuimarisha umoja na Ushirikiano baina
Yao kama iliyoasisiwa na waanzilishi wa TANU na ASP Marehemu
Mwalimu Julias Kambarage Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume ambapo misingi
hio inaendelezwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa kwa sasa Mhe. Dkt.
Samia Suluhu Hassan na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Ali
Mwinyi.
Katika
kukiimarisha chama hicho Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa,
Ndugu Hemed Suleiman Abdulla ameweka jiwe la msingi la tawi la chama hicho
Makufuli jimbo la welezo , tawi la CCM Mtopepo na kushiriki ujenzi wa
Soko dogo Chuwini na ujenzi wa Tawi la CCM jimbo la Mwera Mwembe Mchomeke.
Aidha
Mhe. Hemed amewataka Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi kuunga mkono juhudi
zinazochukuliwa na Viongozi wakuu wa chama Cha Mapinduzi katika kuitekeleza
vyema ilani kwa kuwaletea Maendeleo Wananchi wake ikiwemo ujenzi wa miradi
mbali mbali ya kimaendeleo.
Mjumbe
huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Makamu wa Pili
wa Rais wa Zanzibar amesema Tanzania inapiga hatua kubwa ya maendeleo kutokana
na dhamira njema ya Viongozi wake wenye chachu ya mabadiliko kwa wananchi wao.
Akizungumza
usajili wa kadi za chama kwa njia ya eletroniki Mjumbe huyo wa kamati Kuu ya
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Amesema Dhamira ya Chama Cha Mapinduzi ni
kuhakikisha wanachama wote wanasajiliwa katika Mfumo huo ambao utakuwa na
taafira zote za msingi za mwanachama .
Aidha
Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa amewakumbusha
wanachama kulipa ada za uanachama ili kukiendeleza Chama hicho.
Sambamba
na hayo mjumbe huyo wa kamti kuu ya halmashauri kuu ya ccm taifa ameeleza
kuwa chama cha mapinduzi na Uwongizi hakitamfumbia macho mtu yoyote ambae
atakwenda kinyume na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa lengo la kukichafua Chama
kwa maslahi yake binafsi ama watu wachache wasikipendelea mema chama hicho.
Aidha
amekemea vikali wale wote walionza chokochoko za kupanga safu za uongozi hasa
wabunge na wawakilishi na kusema kuwa muda wa kufanya hivyo haujafika na badala
yake watumie muda wao kuzidi kukiimarisha chama kuanzia ngazi ya Shina hadi
Taifa.
Aidha
amewataka Viongozi wa majimbo kusimamia jukumu lao la msingi waliopewa na
Chama Cha Mapinduzi la kuwatumikia na kuzishirikisha Kamati za Siasa katika
mipango ya maamuzi ili kurahisisha utatuzi wa changamoto zinazowakabili
wananchi wao.
Katika
Ziara hiyo ya kukijenga chama mjumbe huyo wa kamati kuu ya halmashauri kuu ya
CCM taifa Ndugu Hemed ameshiriki ujenzi wa soko dogo LA chuwini linalojengwa
kwa mfuko wa jimbo pamoja na ujenzi wa tawi la CCM Mwembe Mchomeke
Nae Katibu wa
Itikadi na uwenezi Ndugu.Khamis Mbeto amewataka wanachama wa CCM kuachana
na tofauti zao na kuacha makundi yasio na tija katika chama na kuelekeza
nguvu zao zote katika kuwatumikia na kutekeleza ahadi zao kama ilani ya Chama
Cha Mapinduzi Inavyoelekeza.
Amesema
mgawanyiko katika chama ni jambo la kukemewa kwani hautakiimarisha chama bali
utazorotesha mipango ya Chama Cha Mapinduzi na Serikali kwa ujumla .
Nao viongozi wa
majimbo wamempongeza mwenyetiki wa Chama Cha Mapinduzi Taifa ambae
pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia
Suluhu Hassan na Mkamu mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambae pia ni Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa
kuisimamia vyema ilani ya chama hicho kivitendo.
Hata hivyo viongozi hao
wameishukuru serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwaletea maendeleo wananchi
yake pamoja na kuwajengea miradi mbali mbali ya kimkakati katika majimbo yao..
Ziara
hiyo ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Ndugu Hemed
Suleiman Abdulla ametembelea jimbo ya Mfenesini, jimbo la Mwera na Jimbo
la Welezo pamoja na kuweka mawe ya msingi kwenye Matawi ya chama hicho, ikiwa
na lengo la kuimarisha Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake.
0 Comments