Ticker

6/recent/ticker-posts

Wahariri Waongozeni Vyema Wanahabari Vijana

 


Na Nafda Hindi:

WAHARIRI wa vyombo mbalimbali vya habari wametakiwa kutumia nafasi zao  kuwasaidia waandishi wa habari vijana kwa lengo la kuleta maendeleo nchini.

Akizungumza na wahariri Mkurugenzi wa TAMWA,ZNZ Dk Mzuri Issa amesema wahariri wana nafasi kubwa ya kuwaongoza na kuwaelekeza waandishi  vijana katika utendaji wa kazi zao ili waweze kuleta tija kwa jamii na taifa kwa Ujumla.

Dk Mzuri amesema katika kuhakikisha vijana wanafanyakazi  nzuri lazima wahariri watowe mashirikiano ya kutosha na kuwaonesha njia ambazo zinaweza kuwasogeza mbele katika kuleta maendeleo kwa mtu mmoja moja na Taifa kwa ujumla pamoja na kuiletea sifa nchi ya Zanzibar.

Aidha amewasihi waandishi wahabari vijana kuwaheshimu viongozi wao wa Taasisi na kufanya kazi kwa mashirikiano ya pamoja kwa lengo la kujifunza na kuchota ujuzi zaidi kutoka kwao.

Mapema Afisa anaeshuhulikia mradi wa kuwaezesha waandishi wahabari vijana Tatu Mtumwa amewahakikishia wahariri wa vyombo vya vyombo vya habari kuwashirikisha ipasavyo kuwasaidia vijana katika kazi zao za Uandishi ili kufikia malengo yaliokusudiwa.

Nao wahariri kutoka vyombo tofauti wamesema wana kazi ya ziada ya kuzipitia na kuzifanyia masahihisho habari wanazoletewa katika vyumba vyao vya habari hivyo wamewaomba waandishi wahabari vijana kujituma na kusikiliza miongozo sahihi unayopewa na waliokutangulia katika fani hiyo.

Afisa Ufatiliaji na Tathmini kutoka TAMWA,ZNZ Mohamed Khatib Mohamed amewaomba wahariri wa vyombo vya habari waandae utaratibu maalum wa kufatilia habari zinazotoka kupititia vyombo vyao vya habari zinaleta mabadilko katika jamii.

Salim Said Salim ambae alikuwa ni Jaji Mkuu wa kuzipitia na kuzichambuwa kazi za waandishi vijana zilizoshindaniwa katika Tunzo ya kuandika habari za wanawake na Uongozi amesema baadhi ya kazi zilizopelekwa kushindaniwa hazikuwa na vigezo hivyo ni jukumu la wahariri kuzipitia kwa kina na umakini wa hali ya juu habari ambazo zinawasilishwa katika vyombo vyao.



Imane Duwe ni Mkufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar {SUZA) Idara ya Mawasiliano amesma ni vyema kwa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake TAMWA.ZNZ kuandaa mafunzo maalum kwa waandishi wahabari wanawake namna ya kuweza kutumia vifaa kama vile vifaa vya kurikodia sauti na picha wakati wa kuandaa kazi zao

Hata hivyo waandishi wahabari vijana wamesema wanakabiliwa na changamoto kadhaa wakati wa kutayarisha kazi zao ikiwemo mashirikiano madogo kwa baadhi ya vyanzo vya habari wakati wa kukusanya taarifa na kwenda kuzifanyia kazi.

Mkutano huo wa siku moja uliwashirikisha wahariri wa vyombo mbali mbali vya habari kutoka Zanzibar pamoja na waandishi wahabari vijana wenye lengo la kushajihisha waandishi kujikita zaidi kuandika habari za wanawake na Uongozi ulioandaliwa na TAMWA.ZNZ kwa kushirikiana na Ubalozi wa NORWAY.  

Post a Comment

0 Comments