Ticker

6/recent/ticker-posts

Muhali Wa Kutotonzana Faini Ni Donda Ndugu Kwa Vikundi Vya Ushirika Zanzibar


 

Nafda Hindi , Zanzibar

Katika kuhakikisha kwamba watu wenye ulemavu wanaondokana na utegemezi TAMWA ,ZNZ kwa kushirikiana na Shirikisho la J umuiya ya watu wenye ulemavu Zanzibar (SHIJIWAZA) wameandaa utaratibu maalum wa kukusanya vikundi vya Ushirika kwa watu hao venye lengo la kuweka na kukopa na kupata akiba itakayowawezesha kutatua matatizo madogo madogo yanayowakabili katika hali ya kiuchumi.

Watu wanaoishi na ulemavu ni miongoni mwa wanufaika wakubwa wa mradi wa Kijaluba Isave unatekelezwa kwa majaribio katika Wilaya ya Kusini kwa Unguja na Chake Chake kwa Pemba Maafisa mradi wa KIJALUBA ISAVE kutoka TAMWA,ZNZ wamepata nafasi ya kuvitembelea vikundi hivyo katika Wilaya ya Kusini Unguja kwa lengo la kutoa taaluma juu ya masuala ya kuweka na kukopa pamoja na sheria zake zitakazo waongoza kufikia malengo yao waliojiwekea.

Vikundi vilivyotembelewa ni pamoja na TUSHIKAMANE kutoka Muungoni chenye wanachama 19 wanawake tisa (9) na wanawake kumi na moja(11), TUJIGOMBOWE, kutoka Nganani Makunduchi, chenye wanachama ishirini na mbili (22) wanawake kumi na tisa (19) na wanaume watatu(3) na JUMUISHO

kutoka Nganani chenye wananchama ishirini na nne(24) wanawake ishirini (20) na

wanaume wanne (4). Vikundi vyote hivyo vilivyofikiwa na Maafisa Miradi kwa pamoja wamesema vinakabiliwa na changamoto ya uelewa mdogo kuhusu masuala ya utunzaji wa fedha ikizingatiwa kwamba katika ushirika sekta hiyo ni njeti inayohitaji taaluma ya hali ya juu.

“Tumeanza katika vikundi lakini bado hatuna Elimu yeyote kuhusu utunzaji wa fedha kwa hiyo tunahitaji taaluma hiyo ili tuweze kusonga mbele harakati za uwendeshaji wa vikundi,” alisema Amina Haji Seti, mshika fedha kutoka kikundi cha JUMUISHO,Mapema msimamizi wa vikundi kutoka ukanda wa Makunduchi Is haka Mohammed Kheri amesema utunzaji wa fedha ni kikwazo kinachowasumbuwa wana vikundi katika ujazaji wa taarifa zao na kugundua mapungufu kadhaa ambayo yanahitajika kufanyiwa marekebisho.

“Katika suala la ujazaji katika masuala ya fedha tunagunduwa makosa mengi na ii inatokana na wahusika kutokuwa na taaluma ya kutosha katika eneo hili,” alisema Maalim Is-haka.

Hata hivyo alizungumzia suala la kuoneana muhali kwa upande akutonzana faini katika sheria za adhabu ni jambo linalojitokeza katika vikundi vya Ushirika wakati fedha zinazoingia za faini ndio sehemu ya mfuko wao wa mkopo.

Mradi wa KIJALUBA ISAVE inwaotekelezwa kwa pamoja na TAMWA.ZNZ kwa kushirikiana Shirikisho la Jumuiya ya watu wenye ulemavu Zanzibar (SHIJIWAZA) ni mradi wa majaribio katika Wilaya mbili, Kusini kwa Unguja na Chake Chake kwa Pemba.

Post a Comment

0 Comments