Ticker

6/recent/ticker-posts

Mbunge Pondeza Atinga Eneo Litakalojengwa Kituo Kipya Cha Polisi Chumbuni

 


Mbunge wa wananchi wa Jimbo la Chumbuni (CCM) Ussi Salum Pondeza ameambatana na Maafisa waandamizi wa Jeshi la Polisi Tanzaniakulitembelea na kulikagua  eneo lililo kuwa kituo kidogo cha polisi Chumbuni ili kujiridhisha kuwa ni sehemu sahihi ya kujenga kituo kipya Cha polisi.

 

Azma ya ujenzi wa kituo hicho ni kukizi mahitaji  ya wananchi wa Jimbo hilo na maeneo jirani, na ikijulikana kuwa eneo hilo ni karibu na  hospitali ya Wilaya iliyopo Chumbuni.

 

Hatua hiyo ya Kutaka kuanza kwa ujenzi Wa kituo hicho ni Kufuatia maelezo ya Mbunge Pondeza Kupitia Wizara ya Mambo Ya Ndani Ya Nchi kwenye vikao vya  Bunge Jijini Dodoma.

 

Ujenzi huo unaotarajiwa kuanza hivi karibuni Chini Ya Wizara Ya Mambo Ya Ndani Ya Nchi  Na Nguvu Ya Mbunge Wa wananchi Wa Jimbo la Chumbuni Ussi Salum Pondeza .


Post a Comment

0 Comments