Katika kuelekea maadhimisho ya siku ya
mtoto wa Afrika mwakas 2023 Chama cha wandishi wa habari Tanzania kwa upande wa
Zanzibar kimesema licha ya kuwepo kwa sheria ya ya kumlinda mtoto namba 6 mwaka
2011 lakini inaonekana bado vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia kushamiri
siku hadi.
Akizungumza na viongozi mbalimbali walezi, wazazi na watoto katika madhimisho hayo mwenyekiti wa chama hicho Asha Abdi amesema ipo haja ya wazazi na walezi kushirikiana kikamilifu katika kuhakikisha haki za mtoto zinalindwa na kutunzwa katika kumkinga na vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia.
“Sasa hivi dunia ni pana kiteknologia hivyo watoto watumie ipasavyo kwa malengo mazuri na kuhakikisha haki ya motto inapatikana kwa kujifunza mambo mema yanayopatikana katika utandawazi kama vile kujisomea,”alisema.
Nae mkaguzi wa polisi mkuu wa dawati la jinsia mkoa wa kusini Unguja Sadiki Ali Sultani amesema kwa kutumia teknolojia watoto wanaweza kujifunza jinsi ya kutatua matatizo kwa njia mpya naza kiubunifu.
“ Matumizi ya Mtandao ni fursa ,Kwa
mujibu wa sheria ya ushahidi no 9 inatambuwa ushahidi wa kielectronik unatumika
Mahakamani hivyo mtu akitumiwa video au picha ya udhalilishaji
asiisambaze,”alisema.
Akisoma risala katika madhimisho hayo Minna Amour Haji kutoka baraza la vijana wilaya ya kusini Unguja wameiomba jamii kuacha tabia ya muhali katika kuripoti kesi za udhalilishaji wa kijinsia katika vyombo vya sheria.
Sisi watoto tunaiomba Serikali kuhakikisha Taasisi zote zinazosimamia masuala yote ya Sheria kuimarisha hatua za ulinzi mfumo wa Mahakama ili kupunguza mzigo wa ushahidi,”alisema.
Siku ya mtoto wa Afrika huadhimishwa kila ifikapo 16 June ya kilamwaka ambapo chama cha wandishi wa habari wameadhimisha siku hiyo katika ukumbi wa Raha leo Zanzibar kauli mbiu ya mwaka huu ni “Matumizi Sahihi Ya Kidijital Kwa Ustawi Bora Wa Mtoto”.
0 Comments