Mkurugenzi wa Idara ya Watu wenye Ulemavu Zanzibar Bibi Abeda Rashid Abdulla |
Na Ahmed Abdullah
Wakati Dunia
ikiendelea kupigania haki za watu wenye ulemavu visiwani Zanzibar baadhi ya
watu wanaendelea kuwa na mtazamo potofu unaoonesha kuwa watu wenye ulemavu
hawawezui kufanya kazi kama watu wengine wasiokua na ulemavu.
Mtanzamo huu potofu
unaendelea kuenziwa na kizazi hadi kizazi na kuufanya kuendelea na inaamini
imekua ikiwaathiri kisaikolojia watu wenye ulemavu kwa namna moja au nyegine na
kupelekea baadhi ya kukata tamaa kabisa na kubaki kuwa watu wanaosubiri kudra
za Muungu.
Licha ya mtazamo huu
potofu kwa baadhi ya watu lakini Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na wanaharakati
imekua ikisimama imara kupingana na jambo hili kwa kutoa fursa sawa kwa watu
wenye ulemavu na inapobidi hutazamwa wao zaidi hususan kwenye sekta ya ajira.
Katika siku za hivi
karibuni mtendaji mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Hemed Suleiman alikiri
mna kusema watu wenye ulemavu ni muhimu na wachapa kazi zaidi maofisini
wanapopatiwa fursa
Alisema Watu Wenye
Ulemavu wana nguvu na uwezo mkubwa wa kufanya kazi kama walivyo Watu wengine
kwenye uwajibikaji, lakini kinachohitajika kwa Jamii inayowazunguuka ni
kukubali kuwapa dhamana kwa mujibu wa Maarifa, Elimu na Vipaji walivyobarikiwa.
Hata hivyo Mh. Hemed
alisema Watu hao wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbali mbali ndani ya Jamii
hasa lile la kudhalilishwa kijinsia na matokeo yake hubaguliwa na kudharauliwa
mambo yanayokwenda kinyume na haki za Binaadamu.
Alisema wakati
Serikali ikiendelea na wajibu wake katika kuzingatia utatuzi wa changamoto za
Watu hao wenye Mahitaji Maalum, Wananchi pamoja na Taasisi za Kijamii lazima
zifikie maamuzi ya kuondosha manyanyaso hayo kwa kuwapatia fursa wanazostahiki
ili nao wajihisi kuwa sehemu ya Jamii.
Akizungumza na mwandishi
wa Makala hii Akitoa Mkurugenzi wa Idara ya Watu wenye Ulemavu Zanzibar Bibi
Abeda Rashid Abdulla alisema kuna mafanikio makubwa kwa kiasi hususani haki za
watu wenye ulemavu,akitolea mfano miaka ya nyuma ilikua si jambo la kawaida
kumkuta mtu mwenye ulemavu ameajiriwa ofisini.
Alisema hivi sasa kwa
mujibu wa takwimu zao watu wenye ulemavu takribani kila wizara wapo na
wanafanya vyema kuliko mtazamo potofu walionao baadhi ya watu.
‘’Kuendelea kufanya
kwao vyema huku ni kielelzo tosha kuwa watu wenye ulemavu wanachapa kazi na ni
watu wanaopaswa kuthaminiwa’’aliongezea.
Mwandishi pia
amezungumza na mmoja kati ya mtu mwenye ulemavu Juma Kheri alisema yeye binafsi haoni kama ulemavu wake
ni sehemu ya kukos fursa bali ulimpa ari kuongeza bidii ili afanye vizuri tangu
akiwa darasani.
Alisema bidiii hiyo
ndio iliomfanya afaulu vizuri na kupata nafasi ya ajira yenye uhakika,pamoja na
hayo aliwataka watu wenye ulemavu wote kuongeza bidiii na kuonesha uwezo
wanapopata fursa.
0 Comments