Ticker

6/recent/ticker-posts

Wadau wataka marekebisho sheria ya adhabu wanaoficha watoto wenye ulemavu

 

Bi Salma Sadat.

Na Ahmed Abdulla

Wadau mbali mbali wa haki za watu wenye ulemavu wamesema ipo haja kutazamwa tena sheria hiyo kwani kuna baadhi ya changamoto ambazo zinaonekana kuhitaji mabadiliko.

Wameyasema hayo wakati walipokua wakizungumza na mwandishi wa habari hizi alietaka kujua kama wameona mapungufu ya sheria hizo ili ziweze kufanyiwa kazi.

Mmoja wa wadau hao ambao ni Mkurugenzi wa Baraza la watu wenye ulemavu Zanzibar Bi Salma Sadat alisema vipo vipengele vingi vya sheria ambavyo vinahitaji kufanyiwa maboresho.

Akivitaja vipengele viyo Bi Salma alisema alisema ni pamoja kipengele na 42 ambacho kimesema ‘’mtu yoyote atake mficha mtu mwenye ulemavu  atakua ametenda kosa akitiwa hatiani atalipa faini shilingi elf hamsini au isiozidi laki tano za kitanzania.  ‘’

Bi Salma anasema hukumu hii ni ndogo sana kulingana na mazingira halisi,jamii inapaswa kutambua kuwa kumficha mtu mwenye ulemavu ni kumnyima haki zake za msingi ikiwemo kupata elimu.

Alisema mtu mwenye ulemavu ni sawa na mtu mwengine hivyo anapaswa kupata haki zote za msingi kama mtu mwengine.

Alisema wamekua wakipokea kesi ambazo si kwa kiasi kikubwa bado baadhi ya wazazi na walezi wamekua wakiwaficha watu wenye ulemavu majumbani mwao jambo ambalo alisema linapaswa kulaaniwa na kupingwa vikali.

Mmoja miongoni mwa mzazi ambae mtoto wake ana ulemvu anaeishi kisauni Wilaya ya Magharib B Unguja Rashid Maalim aliwataka wazazi na walezi wenzake kuacha kuwafungia watu wenye ulemavu majumbani.

Alisema kuwafungia watu wenye ulemavu majumbani ni kitendo kibaya pia kinapingwa na dini zote kwa sababu hivyo hakina budi kuachwa na jamii kubalika.

Kupitia vyombo vya habari miezi kadhaa nyuma iliripotiwa habari katika kituo cha ZBC kipindi cha mawio ambacho kilifichua mtoto anaeifichwa ndani na kuleta mshangao mkubwa kwa jamii.

 

 

 

Post a Comment

0 Comments