Na Ahmed Abdalla
Imelezwa kuwa Uhuru wa
kujieleza ni jambo muhimu katika kila Taifa linalohitaji kupiga hatua zaidi
katika sekta mbali mbali.
Kauli hiyo imetolewa na
Mkurugenzi wa TAMWA-ZNZ Dkt,Mzuri Issa wakati wa mkutano maalumu uliojikita
kuipitia sheria ya habari visiwani hapa huku lengo kuu likiwa ni kutoa
mapendekezo katika upatikanaji wa sharia mpya.
Alisema jamii ikiwa huru
kutoa mawazo yao ndio njia muhimu ambayo watu hupata kuyasema yale ambayo wengine
wanadhani hayapaswi kusemwa huku wakitumia fursa hiyo kukandamiza wengine au
kuficha mabaya yao.
Wakati mkurugunzi huyo
wa TAMWA-ZNZ akiyasema hayo mratib wa Baraza la Habari Tanzania (MCT)upande wa
Zanzibar Shifaa Said Hassan alisema kuna haja kubwa sana watu kuwa huru kutoa
maoni yao ingawa uhuru huo pia unapaswa kuheshimiwa na kutowakashifu wengine.
Alisema iwapo sheria bora
ya habari itapatikana Zanzibar ana imani mengi zaidi ya kimaendeleo yanaweza
kutokea ikiwemo watu kuelimika zaidi kwa
kujifunza kupitia wengine.
Sambamba na hayo
aliitaka jamii kwa ujumla iwapo sheria mpya iatakayokuja itatoa uhuru wa
kujieleza watu hawana budi kuutumia uhuru huo vyema na kuepuka kujingiza kwenye
matatizo zaidi ya kisheria.
‘’Kupewa uhuru wa
kujieleza hakumaanishi mtu ama watu watukane au kukashifu wengine badala yake
wanapaswa kuutumia uhuru huo vizuri kwa maslahi ya Taifa.
Awali wakichangia
katika mkutano huo miongoni mwa wadau katika sekta ya habari walisema
wanatamani sana kuona sheria mpya ya habari inapatikana visiwani hapa kwani
iliopo sasa haiendani na mazingira ya binadamu wa karne hii.
Miongoni mwa wadau hao
ni mwandishi wa habari wa kujitegemea Tallib Ussi alisema Zanzibar kama Mataifa
mengine ulimwenguni kwa sasa isingepaswa kutumia sharia ya habari yenye
changamoto za hapa na pale.
Alisema sheria
inayohitajika sasa ni hile ambayo haitaacha chembe ya hofu kwa wadau na
wananchi kwa ujumla huku ikiviacha vyombo vya habari na wananchi kwa ujumla
kutumia haki zao za kikatiba ikiwemo ya uhuru wa kujieleza pamoja na kupokea na
kutoa habari.
0 Comments