Ticker

6/recent/ticker-posts

Wadau Wataka Mabadiliko Sheria Ya Usajili Wakala Wa Habari


 

Na Ahmed Abdulla

 

Wadau wa habari visiwani Zanzibar wamesema kuna haja ya mabadiliko ya sheria ya habari visiwani hapa ikiwemo sheria ya Usajili wa Wakala wa Habari, Magazeti na Vitabu namba 5 ya mwaka 1988 kama ilivyorekebishwa na sheria namba 8 ya mwaka 1997

Waliyasema hayo katika mkutano wa siku moja ulioandaliwa na TAMWA-ZNZ kwa kushirikia na Internews Tanzania huku lengo kuu likiwa ni kutazama baadhi ya changamoto za sheria hio.

Awali akiwasilisha mada mtalaamu wa maswala ya habari visiwani hapa Hawra Mohamed Shamte alisema kupitia sheria hio tume ya utangazaji Zanzibar  ina uwezo mkubwa wa kudhibiti  maudhui/habari zinazotolewa na vyombo vya habari vya kielektroniki. Hivyo, nguvu hizo zinaweza kuathiri uhuru wa 18,vyombo vya habari katika utafutaji na usambazaji wa habari.

 

Akitolea mfano alisema kifungu 7(1) (b): Kudhibiti na kusimamia shughuli za utangazaji ,tume imepewa uwezo mkubwa wa kudhibiti mwenendo wa mtangazaji iwapo itaona kwa maoni yake mwenendo wake hauiridhishi Tume.

Alisema neno  ‘kudhibiti’ lifutwe. Sehemu inapaswa kusomeka  ‘kusimamia shughuli za utangazaji.’ Sio kudhibiti

Sambamba na hayo mtalamu huyo pia alisema neno ‘usalama’ lifutwe.’ Sehemu hiyo isomeke: “kulinda sera, utamaduni, mila na desturi za Zanzibar”

 

Wakichangia mafunzo hayo baadhi ya washiriki walisema kwa dunia ya sasa taasisi au mamlaka kupewa nafasi kubwa ya kudhibiti ni kuminya uhuru wa watu kupata habari.

Miongoni mwa wadau hao ni Shadida Ali Omar alisema yawezekana kwa miaka ya nyuma watu walitunga sheria hio lakini hawakutazama mbali zaidi kwa kipindi hicho.

Alieleza kuwa kwa wakati ulipo sasa si sahihi kuwa na sheria ngumu kiasi hicho ambazo zinakandamiza uhuru wa habari.

Alisema sheria inapaswa kuweka wazi na kutoa kipao mbele zaiid haki ya mtu kupata na kutoa taarifa kuliko upande mmoja kujimilikisha kama kwamba wengine hawana haki.


Post a Comment

0 Comments