Jeshi la Polisi Mkoa
Wa Kusini Unguja bado linaendelea kumsaka ndugu. Khamis Abdalla Abdalla mkaazi
wa Ndijani Mseweni aliyekimbia baada ya kutuhumiwa kumlawiti mtoto wa kiume
mwenye umri wa miaka tisa ambaye anasoma darasa la tatu jina limehifadhiwa.
Tukio hilo lilibainika
Julai 30 mwaka huu nchana kweupe huko Ndijani Mseweni wilaya ya kati huku
ikidaiwa kuwa mtuhumiwa huyo ameshafanya matukio kama hayo kipindi cha nyuma.
Baba mzazi wa mtoto
huyo aliema mara baada ya kugundua kuwa mtoto wake huyo katendewa itendo hicho
moja kwa moja alimfikisha hospitali kwa ajili ya vipimo na akagundulika kuwa ni
kweli ameshafanyiwa kitendo hicho kiovu.
“kaonekana kwa macho
ndani ya nyumba mimi nilipoletewa mtoto skumkosha nikaenda nae hospitali mnazi
mmoja baada ya vipimo Daktari akaniambia mwanangu kaingiliwa kinyume na
maumbile” alisema baba wa mtoto huyo
Alisema machungu
wanayopita wazazi wanaopatwa na majanga hayo ya kudhsaaslilishiwa watoto wao ni
makubwa hivyo huku akiviomba vyombo vya sheria kuchukuwa hatua stahiki kwa watu
wanaotenda matendo hayo.
“mimi mwenyewe tokea
jana sijaweza kula chakula chohote wa sijapata usingizi kutokana na kitendo
alichofanyiwa mwanangu/’ Aliongezea baba huyo
Massoud Said Abdalla
ni sheha wa shehia ya Ndijani mseweni alisema jambo hilo halitaki kuvumiliwa
huku akisema kuwa ameshawapanga askari jamii wa shehia hiyo kuendelea kumtafuta
mtuhumiwa huyo ili kumfikisha kwenye vyombo vya sheria.
“baada ya upata
taarifa hii nimeshawaelekeza askari jamii ili kumkamata na kumpadisha
mahakamani” alisema sheha huyo
Kwa upande wake
kamanda wa polisi mkoa wa kusini unguja kamishna msaidizi wa polisi Suleiman
Hassan Suleiman amesema walipata taarifa ya yukio hilo la ulawiti ambapo
walimsaka mtuhumiwa huyo ila alikimbia mara tu baada ya kutenda kosahilo.
“mtuhumiwa alikimbia
na juhudi za kumtafuta zinaebdelea ili kumfikisha katika vyombo vya sheria”
alosema kamanda huyo
0 Comments