Ticker

6/recent/ticker-posts

Waandishi Ongezeni Juhudi Za Kuhamasisha Upatikanaji Wa Sheria Mpya

 


Na Thuwaiba Habibu ,Zanzibar 


Afisa mradi kutoka TAMWA-ZNZ Zaina Mzee wamewataka waandishi kuongeza juhudi na nguvu kwa kushirikiana na wadau wa habari ili kupata sheria rafiki ya habari Zanzibar. 

Hayo yameelezwa katika kikao cha mrejesho wa Mradi wa mapitio ya sheria za habari kilichofanyika ofisi za TAMWA Tunguu Zanzibar chenye lengo la kuwataka wadau wa habari kuzidisha uchechemuzi na ushawishi kwa serikali ili kuweza kupata uhuru wa habari na wakujieleza.

Amesema mradi huo umefikia mwishoni ni muhimu kwa waandishi wa habari na wadau wa habari kushirikiana katika kuhakikisha sheria inapatikana .

Afisa huyo ilieleza kuwa juhudi za ushawishi zilizofanywa, ikiwa ni pamoja na mikutano na baadhi ya Wawakilishi wa Baraza la Wawakilishi, mafunzo kwa wanahabari kuhusu sheria za habari, na kampeni za uelimishaji kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

Aidha amesema, programu hii iliwawezesha waandishi 25 kutoka Unguja na Pemba kupata mafunzo ya kina juu ya sheria ya habari.

Kaimu Mkurugenzi kutoka TAMWA-ZNZ Bi shifaa Said Hassani amesema safari hii ya kutaka kupata sheria rafiki ya habari ni ya takribani miongo 2 na kwa sasa tumepiga hatua kwa kupata mafanikio ambayo kutokana na mchango wa kila wadau na waandishi.

"Kwa sasa kila mtu anajuwa uwepo wa kutamani sheria rafiki kwa waandishishi hapa visiwani"

Wanashukuru uwepo wa mradi huu kuweza kuwapatia elimu waandishi kuelewa umuhimu wa kuwa na sheria rafiki na uhuru wa kujieleza 

Pia amesema wadau na waandishi waendelee kushirikiana na kulifanyia kazi suala la kupata sheria ya habari

Kwa upande wake Afisa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka TAMWA, ZNZ, Mohammed Khatib, alisema kuwa mkutano huu ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha uwazi, ushirikishwaji na kuimarisha sauti ya wanahabari katika mchakato wa mabadiliko ya sheria za habari.

“Kwa kipindi chote cha utekelezaji wa programu hii, tumeweza kufikia hatua muhimu katika kuhamasisha majadiliano ya kina kati ya waandishi na wadau wa habari na watoa maamuzi. Ripoti tunayowasilisha leo inaonesha hali halisi, mafanikio, lakini pia maeneo yanayohitaji maboresho,” alisema 

Nao washiriki na wadau wa habari walitoa mbinu mbali za kutumia ili kurahisha upatikanaji wa sheria hiyo na pia walishukuru kutatiwa mafunzo ambayo yamewawezesha kupata ulewewa wa sheria za habari na kuandika kazi hizo za uweledi.

Post a Comment

0 Comments