Na
Berema Suleiman:
Sheria ya Wakala wa Habari, Vitabu na Magazeti namba 5 ya mwaka 1988, iliyofanyiwa marekebisho kwa Sheria
Na. 8 ya mwaka 1997, ni moja kati ya sheria zinazotumika kuendesha shughuli za
vyombo vya habari Zanzibar.
Moja wapo ya
vifungu vyake vinavyokosolewa kwa kiasi kikubwa na wadau wa habari ni Kifungu cha 30(1), ambacho kinampa
mamlaka Waziri mwenye dhamana ya habari kusimamisha chapisho au gazeti lolote
kwa madai ya maslahi ya umma au usalama wa taifa.
Vifungu hivi
vimeibua mjadala mpana miongoni mwa wanaharakati wa haki za binadamu, waandishi
wa habari pamoja na wanasheria kwa kutaka kufaanyiwa marekebisho ya
sheria mpya yaa habari kwa maslahi ya tasnia ya habari na taifa kwa ujumla.
Kifungu hiki
kinaeleza kuwa:
“Waziri anaweza, kusimamisha kwa
muda au kuzuia kwa ujumla uchapishaji au usambazaji wa gazeti a ikiwa ataona
kuwa maudhui yake yanaweza kuhatarisha usalama wa taifa, amani ya umma, au
maadili ya jamii.”
Hii ina
maana kuwa Waziri wa Habari anaweza, bila kuhitaji kibali cha mahakama, kutoa
amri ya kusitisha gazeti kutokana na tathmini yake binafsi juu ya yaliyomo
kwenye chapisho hilo.
Makala hii
ilizungumza na wanasheria ambae pia ni wakili waa kujitegemea Thabit
Abdalla alisema kuwa kifungu hiki kinaipa serikali mamlaka makubwa mno
yanayoweza kutumika vibaya dhidi ya uhuru wa vyombo vya habari.
“Sheria hii
ni ya zamani na inakiuka misingi ya utawala bora na uwajibikaji. Waziri anakuwa
na mamlaka ya mwisho, bila nafasi ya gazeti au mmiliki wake kujitetea. Hili
linakiuka haki ya kusikilizwa na misingi ya haki za binadamu,” alisema Thabit.
Alieleza
kuwa, katika nchi zinazoheshimu demokrasia, maamuzi ya kusimamisha gazeti
hufanywa na mahakama kupitia mchakato wa wazi wa haki.
Aidha
alisema ni wajibu wa mamlaka husika kuwa mstari wa mbele katikaa kuhakiisha
sheria mpya ya habari inafanyiwa marekebisho ili wandishi wa habri na vyombo
vya habari kufanya kazi kwa weledi katika kutoa tarifa zinazowajibisha
viongozi.
Kwa upaade
wake mjumbe wa kamati ya kitaalaamu ya masuala ya sheria za habari Zanzibar
(ZAMECO) Abdalla Mfaume alisema na kukiri kwamba kutokana na kifungu
hicho kinaathiri uhuru wa habari na vyombo vya haari kuyokanana mamlak makubwa
aliyopewa waziri kaatika kufungia vyombo vya habari ikiwemo magazeti hivyo
alisemaa kuna haja ya kuwa na uwiano kati ya uhuru wa habari na maslahi ya
taifa.
“Ni kweli
tunahitaji mabadiliko ya sheria hii ili kulinda uhuru wa vyombo vya habari,
lakini hatuwezi pia kupuuza athari hasi za maudhui yanayoweza kuleta chuki au
uchochezi,” anaeleza Mfaume.
Hata hivyo,
anashauri kuwe na tume huru ya
habari itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguza na kutoa maamuzi badala ya waziri
mmoja pekee.
Pamoja na
hayo kwa upande wake muandishi wa habari mkongwe Jabir Idrisa, ambaye amewahi
kukumbwa na adhabu ya kufungiwa kwa gazeti alilokuwa analiandikia alisema
iwapo sheria haitafanyiwa marekebisho kwa vigungu vinavyokwaza uhuru wa habari
basi maendeleo hayawezi kuongezeka.
“Sheria hii
imekuwa chombo cha kuua uhuru wa kujieleza. Waandishi wanaandika kwa woga,
wakihofia gazeti kufungiwa. Hii si afya kwa demokrasia,” alisema Jabir.
Anasisitiza
kuwa Zanzibar inahitaji sheria
mpya ya habari itakayoendana na katiba, mkataba wa kimataifa wa
haki za binadamu, na maendeleo ya teknolojia.
Kwa upande
wake mtetezi wa haki za binadamu THRDC Shadida Omar kutoka Mtandao wa
Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) alisema sheria hiyo ni kandamizi
na inakinzana na mikataba ya kimataifa ambayo Tanzania (ikiwemo Zanzibar)
imeridhia, kama vile Mkataba wa
Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa (ICCPR).
“Sheria hii
inatoa mianya ya kudhibiti vyombo vya habari visivyoegemea upande wa serikali.
Tunapaza sauti kudai mabadiliko ya haraka ya sheria hii,” alisema Shadida.
Pia
alipendekeza kusema kuwa kila mmoja ana haki ya kufanya kazi bila ya woga
na hofu katika kutekeleza majukumu yake hivyo ni wajibu wa taasisi husika
kuhakikisha sheria mpya ya habari inapatikana kwa maslahi mapana ya wandishi wa
Habari na vyombo vya habari hapa nchini.
Kwa miaka
mingi, Kifungu cha 30(1) cha
Sheria ya Magazeti na Vitabu kimekuwa chanzo cha mgongano kati ya serikali na
vyombo vya habari.
Wadau
mbalimbali na wandishi wa habari wana mtazamo wa pamoja kuwa, ili kujenga jamii
yenye uhuru wa kujieleza na kupata taarifa, kuna haja ya kuifanyia marekebisho
sheria hii kwa kuzingatia katiba ya Zanzibar, haki za binadamu, na muktadha wa
sasa wa kidemokrasia.
0 Comments