Na Siti Ali, Zanzibar:
FANI ya habari ni kama fani nyengine
inaongozwa kwa sheria na kanuni mbalimbali hivyo waandishi wanapaswa kuzifahamu
sheria na kanuni hizo sambamba na kuzitambua vyema zile sheria na ibara zote
zinazokwaza uhuru wa vyombo vya habari ili waweze kutekeleza majukumu yao
zaidi.
Lakini
waandishi wa habari zanzibar bado wanaumiza kichwa kuhusu marekebisho ya sheria
na hata kuamua kuwa nakauli mbiu “uhuru wa vyombo vya habari na mageuzi ya sera
na sheria za habari zanzibar” katika siku ya waandishi wa habari duniani 2024.
Kwa muda
mrefu (1988) licha ya wadau mbalimbali kutoa na kuwasilisha mapendekezo ya
kutaka mapungufu yaliyopo kwenye baadhi
ya sheria za habari yafanyiwe marekebisho, lakini utekelezaji wake bado umekuwa
wa kusuasua jambo linalopelekea mazingira magumu ya utendaji kazi wa waandishi
wa habari nchini.
Kwa bahati
mbaya kilio cha waandishi wa habari Zanzibar
hakijapata muombezi hadi sasa, hii inatokana na misukosuko wanayokumbana nao
kila siku wakiwa katika majukumu yao ya kila siku.
Wakati wa
maadhimisho ya Uhuru wa Vyombo vya Habari
duniani mwaka 2024, Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake
Tanzania, (TAMWA Znz), Dkt. Mzuri Issa
alielezea kwamba mchakato wa mabadiliko ya sheria za habari umekuepo kwa miaka
mingi lakini bado sheria hizo ambazo nyingi ni za muda mrefu zimekwama
kurekebishwa.
"Sisi
wengine tangu tuko waandishi chipukizi tunazungumzia kupata sheria mpya za habari, tangu 2008 kwa kweli
ni muda mrefu, tunahitaji kusimamia jambo hili kwa umoja wetu hatimae tupate sheria mpya za habari Zanzibar,
“Licha ya
kuwasilisha ripoti ya mapendekezo yao kwa mamlaka husika ikiwemo kukutana na
Rais wa Zanzibar pamoja na waziri anayeshughulikia masuala ya habari,lakini
bado jitihada zetu zinagonga mwamba kwasababu kila mara tunachopewa ni ahadi tu
kwamba sheria ziko mbioni kurekebishwa , " alieleza dkt. Mzuri .
Kikwazo
kikubwa sheria iliyopo haifanani na wakati
uliopo kutokana na ukuaji wa sayansi na teknolojia kwani hivi sasa dunia
umetoka kwenye mfumo wa analogi na
kuhamia digitali hivyo kutoa nafasi ya mambo kufanyika kwa haraka na ufanisi,
Hivyo hata
utendaji kazi na mazingira ya uwendeshaji wa vyombo vya habari umebadilika na
kusababisha sheria zinazosimamia vyombo hivi pia kupaswa kubadilika.
Mwandishi wa Zanzibar anasimamiwa na sheria zisizopunguwa sita
,lakini nyingi zao ni za kudhibiti na
si kumlinda ili aweze kufanya kazi zake
vizuri .
Miongoni mwa sheria zinazompatia mwandishi wa
habari maelekezo namna gani afanye na kutoa Adhabu kwa mfano ukiangaliya sheria
inayoitwa ya Usalama wa Taifa na. 8 Mwaka 2010, Sheria ya Takwimu, na. 9 ya
Mwaka 2015 ,Sheria ya Uchaguzi,na.4 mwaka 2018, na sheria ya Tume ya Utangazaji na. 7 ya Mwaka 1997 iliyofanyiwa
marekebisho na Sheria na.1 ya Mwaka 2010, zote zipo kwa kumpa fursa ya kufanya
kazi lakini hazina nafasi ya kumlinda na kumuendeleza mwandishi wa habari.
“sheria
inayotoa nafasi kwa Waziri au Taasisi ni Sheria ya Usajili wa wakala wa
habari,magazeti na vitabu, ya na.5 ya mwaka 1988 kama ilivyorekebishwa na
sheria na. 8 ya mwaka 1997 ambapo inamtaka
waziri kulifungia gazeti kwa
manufaa ya umma au kwa maslahi ya taifa.kufanya hivyo ni kuingilia kati
mwenendo wa utoaji wa taarifa, utangazaji, uandishi au kufungia na kusitisha
chombo cha habari kisifanye kazi, hali hiyo ikiendelea kuachwa uhuru wa habari
kitanzini ”, amesema Mwinyimvua Abdi Nzuki, katibu wa Klabu ya Waandishi wa
Habari Zanzibar (ZPC).
Mwandishi wa
habari Mkongwe Salim Said Salim alieleza uwepo wa sheria bora ni muhimu katika
kuwezesha mazingira bora ya waandishi wa habari kuwajibika.
"Vyombo
vya habari ni washirika wa maendeleo, hivyo kuwa na sera na sheria bora
itawawezesha waandishi wa habari kuwa na mazingira rafiki katika kutekeleza
majukumu yao," alifahamisha, mwandishi wa habari huyo mkongwe Zanzibbar.
“Nidhahiri
kwamba hakuna sheria rafiki kwa sisi waandishi wa habari kwani hata wakati wa
ufanyaji wa kazi hivyo hutufanya kutokutumiya maadili wakati wa baadhi ya
utekelezaji wa baadhi ya majukumu yetu ya kuihabarisha jamii na kukosekana kwa
usawa wa mafanikio kati yake na wateja wake na kupelekea ukandamizaji wa sheria
na kupata madhara makubwa yanayoweza kuathiri usalama wake” Jesse Mikofu
mwandishi kutoka kampuni ya mwananchi ameelezea.
Jabir Idrisa
Mwandishi wa Habari Mkongwe amekiri kwa kusema kuwa ‘’kutokana na kuwa sheria
za habari zilizopo si rafiki kwa waandishi wa habari hivyo hukabiliwa na
changamoto nyingi zinazowakwaza
kutekeleza majukumu yao.
Miongoni mwa
changamoto hizo ni mwandishi kufungiwa asiandike kwa muda , kuporwa vifaa
vyakevya kazi , kunyimwa uhuru wa kusambaza na kuchukua habari, pamoja na kutishiwa amani”anaeleza Jesse
“Sheria rafiki za habari zinasaidia waandishi wa habari kufanya kazi zao bila ya
hofu wakiamini kwamba sheria zilizopo zinawalinda .lakini kinyume chake
,kukosekana kwa sheria rafiki ,inasababisha hofu kwa waandishi na vombo vya
habari,kunadumaza demokrasia na utawala bora .
“Nchi ambayo
haina sheria rafiki za habari inaweza kuchelewa kupata maendeleo kwa sababu
changamoto zinazowakabili wananchi haziwezi kuibuliwa na kufika haraka kwa
mamlaka husika” ameeleza Juma Khamis Juma (Mwanasheria)
Bishifaa
Said Hassan Mjumbe wa Kamati ya Wataalamu wa Habari Zanzibar (ZAMECO)
tutashirikiana na waandishi wa habari kuongeza kasi ya uchechemuzi na utetezi
juu ya sheria hizi kandamizi kwa vyombo vya habari na waandishi wa habari kwa
ujumla.
Na tunaamini kuwa sauti na kalamu zao zinafika
mbali sana kwa haraka zaidi, hivyo basi ni wajibu kuhakikisha munatumiya kalamu vizuri katika kuhakikisha munaandika habari
na makala mbalimbali juu ya sheria hizi kusudi zifanyiwe maboresho.
Licha ya
kufanyiwa mrekebisho kwa mfano Sheria ya Usajili wa Wakala wa Habari za
Magazeti na Vitabu na. 5 ya Mwaka 1988 iliyofanyiwa marekebisho na kubana zaidi
na Sheria na. 8 ya mwaka 1997 Sheria hizi bado vipo vifungu visivyotoa uhuru wa
kutoa taarifa na kujieleza na kutoa nafasi ya kuuficha ukweli wa jambo kwa
kulinda maslahi ya umma au kwa kulinda amani na utulivu .
Hivyo basi
ni vyema serekali na mamlaka husika kulifanyia kazi suala la sheria za habari
ili kuepusha usumbufu unaotokea kwa vyombo vya habari na waandishi kwa ujumla.
0 Comments