Na Siti Ali, Zanzibar:
MWANDISHI wa habari ni mtu ambaye ana jukumu la kutafuta, kukusanya, kuandika na kusambaza habari kwa wasomaji, wasikilizaji na watazamaji katika jamii. Ili kuifanya vyema kazi yake kwa kuzingatia ukweli, kuepuka kuchukua taarifa feki,kuzingatia usahihi, kutoegemea upande wowote, kuzingatia muda, kufanya usawa katika vyanzo vyake na kujiepusha na vitendo vya rushwa.
Kutokana na majukumu hayo humfanya mwandishi wa habari
kuwa mfano bora na kuwafanya wengine kuwajibika katika ufanyaji wao wa majukumu
ya kila siku. Hii ni pale ambapo kalamu yake inapofanya kazi ya kukosoa kukemea au kushauri hali inayopelekea
serikali kuchukua hatua juu ya jambo lililozungumzwa na mwandishi wa habari.
Licha ya kuuona umuhimu wa mwandishi wa habari katika
jamii lakini pia wapo baadhi ya watu ambao si waadilifu ambao wanawanyima uhuru
waandishi kupata taarifa hali ambayo inarudisha nyuma juhudi zao pamoja na
kumnyima mwanajamii haki yake ya kupata
taarifa .
Tunaelewa kwamba siku zote muungwana ni yule
anayemtafuta mmiliki wa kitu anachokitaka kwa lengo la kupatiwa ridhaa au
baraka na hapa nimewatafuta baadhi ya waandishi wa habari ambao wamekutana na
changamoto hiyo na kusema kuwa.
“Waandishi wa habari visiwani Zanzibar wanakabiliwa na
changamoto kadhaa katika utekelezaji wa majukumu yao ikiwamo kupata vitisho
kutoka kwa viongozi wa serikali, ukiandika chochote kinachohusiana na taasisi
au mamlaka fulanikama haikuwafurahisha kuyaondosha hewani au kuyakana, hali hii
ni ukandamizaji wa haki ya kupata kupata kusambaza habari “amesema Thuwaiba Habibu
mwandishi wa habari wa kujitolea.
“Changamoto nyingi wanazokumbana nazo waandishi wa
habari zinatokana na sheria tulizo nazo
kwa mfano sheria ya Usajili wa Wakala wa Habari ,Magazeti na Vitabu na.5 ya Mwaka 1988 iliyofanyiwa marekebisho na sheria na.8
ya mwaka 1997 na Sheria ya Tume ya Utangazaji ya Mwaka 1997 pamoja na
marekebisho yake Mwaka 2010 .kutokana na vikwazo vilivyomo ndani ya sheria hizo
,waandishi wa habari wanapata hofu kutoa baadhi ya taarifa .” Amesema Thuwaba Habibu
.
Wanahabari wengi visiwani Zanzibar hukosa kutekeleza
jukumu la kupata taarifa na hapa ile kauli ya mjomba nsaidie ndiyo hudhibitika
kwa kuwa vyombo binafsi hukosa fursa sawa na vyombo vya serikali. Kama
alivyoeleza mdau wa habari kutoka visiwani humo, ambapo ndiyo kulikoanza
waandishi wa habari wanawake
“Wanahabari hatuna uhuru katika ufanyaji wa kazi ya
kutafuta taarifa hususani vyombo binafsi ambavyo hukandamizwa na baadhi ya
watumishi wa umma kupitiya nyadhifa walizo nazo” alisema Bakari Haji Khamis mwandishi
wa habari wa kujitolea.
Naye Mauwa Juma Salim mwandishi wa habari wa TIFU TV anaelezea
changamoto wanazokumbana nazo ikiwamo baadhi ya waandishi wa habari kunyimwa fursa ya kuchukua taarifa
muhimu ili kuihabarisha jamii kwa kisingizio cha chombo cha binafsi na badala
yake kupewa fursa mwandishi wa chombo cha serekali hii inamaana ya kwamba uhuru
wa habari haupo kwa waandishi wa habari kutoka vyombo binafsi hivyo kupelekea
wananchi wanaopendelea kusikiliza au kusoma taarifa zinazoandikwa /kutangazwa
na vyombo hivyo , kukosa haki ya kupata taarifa.
“Vile vile wanahabari hatuna uhuru katika ufanyaji wa
kazi ya kutafuta taarifa hususani vyombo binafsi ambavyo kukandamizwa na baadhi
ya watumishi wa umma kupitiya nyadhifa walizo nazo”ameeleza Mauwa.
Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake
Tanzania (TAMWA ZNZ) Dk. Mzuri Issa anasema kama wanahabari wanakosa haki ya
kupata taarifa na jamii haiwezi kupata taarifa zinazowahusu, hivyo inapaswa
utekelezaji wa haki ya kupata habari na
kujieleza kama ilivyo ndani ya Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, (ibara ya 18).na ile iliyomo katika katiba ya
zanzibar kifungu na. 18(1) na (2)
Ibara na.18 (1) kinasema Bila ya kuathiri sheria
nyengine za nchi kila mtu anayo haki ya uhuru wa maoni,kujieleza,kutafuta
kupokea na kusambaza habari na mawazo yake kupitia chombo chochote cha habari
bila ya kujali mipaka ya nchi na pia anayo haki na uhuru wa kutokuingiliwa mawasiliano
yake .
Kutokana na ukongwe wa sheria zilizopo ambazo zinaweka
wajibu wa waandishi wa habari kutafuta taarifa lakini hakuna wajibu wa waajiri wa serikali kutoa
taarifa hizo, inakuwa ni vigumu kwa wanahabari kufanya majukumu yao ya
kuuhabarisha umma habari zisizoegemea upande na habari zenye ukweli usio na
chembe ya shaka .
Fatma Ramadhan Juma pamoja na Juma Mohd wakaazi wa Mfenesini wanasema kuwa
wanachangamoto kazaa ambazo wangependa zijulikane kwa jamii na hata kwa wenye
mamlaka lakini wanashindwa kuzielezea
kwani wamekuwa wakitoa taarifa kwa waandishi lakini hazijapata nafasi ya
kutolewa kwenye vyombo vya habari.
Fatma anasema kuwa hali hiyo inaonesha kuwa kuna
mchujo mkubwa katika vyombo vya habari na taarifa zinazowagusa wananchi moja
kwa moja mara nyingi huwa hazipewi nafasikwa sababu ya woga au kuna watu
wanalinda tonge zao.
“Kila siku tunatoa taarifa kwa waandishi wa habari
lakini tukifuatiliya taarifa tulizotoa hazijatumwa au zikitumwa baadhi ya
maneno yanatolewa ambayo ndiyo malengo yetu tuliyokusudia kwa serikali na
hufanya hivyo kwaajili ya usalama wao”anaeleza bwana Juma.
Kupitia makala hii leo naomba kuwauliza swali hivi
jamii ikikosa taarifa je, kuna mtu anaweza kuishi kwa amani katika dunia hii?
Wakati unafikiriya hilo, napenda kuwakumbusha maneno ya wahenga yasemayo
usimdharau akubebaye na usiangalie ulipoangukia, angaliya ulipotelezea
watumishi wa umma sasa wanabudi la kufikiriya njia nzuri ya kutatua tatizo hili
ili jamii kupata taarifa kwa wakati sahihi kupitiya vyombo vya habari.
0 Comments