Ticker

6/recent/ticker-posts

Jamii Yahimizwa Kulinda Haki Za Watoto
 NA Amrat Kombo, Zanzibar:

Jamii imeshauriwa kutunza na kulinda haki za watoto kwa lengo la kuwapatia maendeleo .

Akizungumza visiwani Zanzibar katika mkutano wa majadiliano  ya haki za watoto na wadau mbalimbali ulioandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kusaidia watoto . 

Afisa wa Hifadhi ya mtoto kutoka shirika hilo  Ahmed Rashid Ali amesema wazazi wanatakiwa kutoa kipaumbele kwa watoto wao bila ya ubaguzi.

" Ni muhimu wazazi kuwapatia watoto wao haki zao za msingi bila ya ubaguzi kati ya mwanamke na mwanaume kwani ni chanzo cha kuwajengea upendo kati yao."alisema Ahmed 

Pia amesema wazazi wanajukumu la kuwalinda watoto wao katika shughuli mbalimbali za kijamii.

" Mzazi anatakiwa kutoa elimu kwa mtoto wake juu ya kujilinda na vitu mbalimbali ikiwemo udhalilishaji wa mitandaoni."Ahmed

" Baadhi ya wazazi hawana desturi ya  kuwapatia elimu watoto wao juu ya kujilinda na udhalilishaji jambo ambalo husababisha mtoto kuthirika na vitendo hivyo." aliongezea 

Nae Afisa Mawasiliano kutoka shirika hilo Usia Nkhoma alisema kuna umuhimu wa kutumia lishe bora ambayo itasaidia kujinda na maradhi mbalimbali ikiwemo kisukari.

Pia alisema ukosefu wa lishe ni chanzo cha udumavu wa watoto pamoja na ukosefu wa damu kwa mama mjamzito.

" Watoto hawapati chakula chenye lishe bora,na  husababisha mtoto kupata maradhi mbalimbali ikiwemo utapia mlo." 

Pia alisema idadi  ya kina mama laki moja  wanaokufa uzazi imepunguwa katoka  134 hadi 9 na hii inatokana na  kufuta ushauri wa daktari.

Sambamba na hayo alisema  idadi ya watoto wanaopelekwa kituo cha afya inaongezeka kutokana na wazazi kufuta taratibu za daktari. 

Aidha alisema idadi ya vifo vya watoto wachanga katika kila watoto elfu 1 imeongezeka kutoka 28 hadi 34 ya mwaka 2016.

"  Takwimu ya mwaka 2019 hadi 20 inasema asilimia 30. 1 watoto hawapati mahitaji ya lazima ikiwemo chakula makaazi pamoja na mavazi.

Baadhi ya wadau wameomba  serikali kueka mazingira uwezeshi ya walimu kwa watu wenye mahitaji maalum.

" Tunaomba watoto wapunguziwe masomo ili wapate kujiandaa vizuri na mitihani yao kwani masomo mengi huwa ni mzigo kwa watoto hao."alisema Nadyah 

Pia amesema ni vizuri watoto wakishirikishwa katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo kwasababu inamjengea uwezo wa  kujiamini.

Aidha alisema kuwepo kwa sera na sheria za  mtoto inasaidia kumlinda na mambo mbalimbali katika jamii.

Post a Comment

0 Comments