Ticker

6/recent/ticker-posts

Dkt. Mzuri "Kaongezeni Uelewa Kwa Wananchi Juu Ya Ushiriki Wa Wanawake Kwenye Michezo"



Na Ahmed Abdulla, Zanzibar:

WAANDISHI wa Habari nchini wametakiwa kuihamasisha jamamii kushiriki kikamilifu katika michezo ili kupatikana usawa wa kijinsia katika sekta hiyo.


Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA- ZNZ), Dk Mzuri Issa alisema hayo alipokuwa akifungua mafunzo ya siku tano ya kuwajengea uwezo waandishii wa habari juu ya kuripoti masuala ya habari zitakazowashajihisha wanawake na wasichana wa Zanzibar kuingia katika michezo.


Alisema kunamapungufu makubwa kwa wanawake kushiriki katika michezo haliambayo inawasababisha kuzikosa fursa mbalimbali.


Dk Mzuri alifahamisha kuwa michezo ni ajira, michezo ni afya na michezo ni chachu ya kukuinua kiuchumi hivyo kunakila sababu ya eneo hilo kutiliwa mkazo ili kuona kundi hilo nalo linashiriki kikamilifu ili kuweza kunufaika nazo.


Sambamba na hayo alisema ushiriki wa mwanamke katika michezo unaweza kuleta mageuzi ambayo yanahitajika katika jamii na kuweza kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu hapa nchini.


Alisema kwa muda mrefu wanawake wamekuwa wakiachwa nyuma katika masuala ya michezo na kurejesha nyuma maendeleo yao, hivyo wakati umefika sasa kwa waandishi kuelekeza nguvu zao katika sekta hiyo ili kuonesha umuhimu wa ushiriki wa wanawake katika michezo ili kuleta mabadiliko.


Mkufunzi wa mafunzo hayo Hawra Shamte alisema mkakati zaidi unahitajika ili kuona wanawake wanashiriki kikamili katika michezo.


Kwa upande wa washiriki wa mafunzo hayo walisema mchezo wa mpira wa miguu kwa wanawake ni ajira kwasababu unawapatia fursaya kwenda kuchezea timu kubwa ziliyopo nje ya nchini.


Mradi huo wa mwaka mmoja michezo kwa maendeleo kwa Afrika unalenga kuwawezesha wanawake na wasichana kupitia michezo Zanzibar unatekelezwa kwa pamoja na TAMWA –ZNZ, ZAFELA na CYD unafadhiliwa na Shirika la Michezo la Ujerumani (GIZ).

Post a Comment

0 Comments