Ticker

6/recent/ticker-posts

Ni Kwa Namna Gani Wanawake Wanaweza Kuwa Viongozi Wa Siasa Majimboni.

 


NA AMRAT KOMBO,ZANZIBAR


WANAWAKE na uongozi, wanawake wanaweza bila ya kuwezeshwa, wanawake ni wajasiri, wanawake ndio wenye uchungu wa maendeleo.

Baada ya mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi yaliyotokea mwanzoni mwa miaka ya 1990 -ukijumuisha na Mkutano wa Beijing kuhusu uwezeshwaji wa wanawake, taratibu kibao kilianza kugeuka.

Kwanza, kuruhusiwa mfumo wa vyama vingi kulimaarisha kutanuka kwa wigo wa wanawake kuwania nafasi za uongozi kupitia vyama vingine vya kisiasa.

Zaidi ya chama tawala cha CCM, wanawake sasa walijitokeza kuwania nafasi katika vyama vya upinzani na kupata fursa ambazo zisingekuwa rahisi kuzipata katika mfumo wa chama kimoja.

Kuruhusiwa kwa asasi za kiraia pia kulifungua njia kwa wanawake kuonyesha uwezo, maono na ujasiri wao kwenye kuhoji na kuishauri serikali kwenye mambo ya maslahi kwa taifa.

Wanawake mashuhuri wa miaka ya 1990 kama vile Leila Sheikh Khatib, Dk. Ananilea Nkya, Mary Rusimbi, Marie Shaba na wengine walipata umaarufu na heshima si kwa kutumia vyama vya siasa bali zaidi kupitia harakati zao kupitia asasi za kiraia.

Kama kuna jambo walilofanikiwa kulifanya wakati ule ilikuwa kuonyesha kwamba wanawake wanaweza kuwa viongozi pasipo kuwa wanasiasa kamili.

Matokeo yake ni kwamba mwaka 2010, Tanzania iliweza kupata wanawake wabunge 23 waliopata nafasi zao kupitia majimbo ya uchaguzi. Ukijumuisha na wale wa viti maalumu, Bunge la Tanzania likafikisha asilimia 29 ya wabunge wanawake -kiwango cha juu kabisa kwa wakati huo.

Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, wanawake wamejitokeza kwa wingi kuwania nafasi mbalimbali za kuchaguliwa kuanzia Urais, ubunge na udiwani.

Chama cha upinzani cha ADC kimempitisha mwanamama Queen Sendiga kuwa mgombea wake wa nafasi ya urais katika uchaguzi huo.

Chama kikuu cha upinzani kimetangaza orodha ya wagombea wake wa ubunge ambako takribani wanawake 35 wamejitokeza kwenda majimboni kuwania ubunge. Idadi hiyo ni zaidi kidogo ya asilimia 20 na ndiyo kiwango kikubwa cha wagombea wanawake kupitishwa na chama hicho kuwania ubunge tangu kuanzishwa kwake..

 Kwa upande wa Zanzibar ,wakati anaingia Ikulu raisi mstafu DKAli Mohmmed Shein mwaka 2010 alianza kwa kuwapa wanawake  nafasi za uwaziri.

Maana wengi walishaota mizizi kwenye akili zao kwamba, wanawake hawapaswi kuonekana kwenye meza refu wakiwa mawiziri.

Kwa miaka mingi tunaona idadi ya wanawake viongozi inaongezeka taratibu kutokana na mitazamo mbali mbali na juhudi zinazochukuliwa, wapo ambao wanaishia njiani kwa sababu tofauti lakini wapo ambao wanapambana hadi kuwa viongozi wa majimbo.

Kauli mbiu ya wanawake na uongozi wakati huo na sasa imeshikiwa bango na wanaharakati kama vile TAMWA, ZAFELA, ZSLC, TGNP, ZAWCO, na mradi wa WEZA na ndio maana idadi ya wanaoibukia majimboni inaongezeka.

Na dhamira hii ya mwanamke kupambana inawavutia wengi na wanaamua kuiga mifano yao hadi na wao kutimiza ndoto zao.

Mwakilishi Mstaafu wa jimbo la Magomeni Hapsa Said Khamis amesema ameingia katika siasa katika kipindi cha mfumo wa vyama vingi mwaka 1995 lakini hakuwahi kukataa tamaa .

" Sikuwa na hofu wakati nagombania kwasababu nilipata ushirikiano katika kijiji changu kuanzai wazee hadi vijana na nikafanikiwa kushinda miaka yote miwili." alisema

 Pia amesema imani ya mtu ndio inayomsabishia mtu kufikia malengo yake.

" Ukiwajengea watu imani wakuamini basi shirikiana nao katika hali yoyote ile itawafanya kuwa na upendo na wewe." alisema hapsa

Samabamba na hayo  amelezea mbinu mbalimbali ambazo zitamsaidia mwanamke kuwakiongozi katika jimbo .

" Kwanza unatakiwa ujitambuwe,uwe na ushirikiano na vyama vyote sio chakwako tu,kila moja uwoneshe unavomjali, ugonvi hautakiwi ,pamoja kuwathamini wazee bila ya kuwajali wazee unaweza kupata mitihani." alisema

 Wanawake wengi ni wavumiilivu na wastamilivu,hawajawahi kukata tamaa katika maisha yao,kwa lengo la kuamini kuwa iko siku wataweza kufanikiwa. Licha ya kuwa kuna baadhi ya watu hujitokeza katika maisha ya mtu kwa lengo la kumuharibia maisha yake.

Moja kati ya mwanamke aliyejitokeza kugombea nafasi ya uwongonzi kwa miaka nne mfululizo  lakini hakuweza kufanikiwa .

Hasni Abeid wa chama cha ACT wazalendo amesema ameanza kugombania tangu 2005 lakini hakuweza kufanikiwa.

" Nilipambana na changamoto mbalimbali ikiwemo vitisho lakini niliendelea kupambana japo haikuwa riski kuweza kushinda nikaendelea kugombea tena uwakilishi 2010 sikuweza kufanikiwa," alisema

"sikuchoka nikagombea tena 2015 sikufanikiwa,na siku kata tamaa 2020 nikagombea tena vilevile sikufanikiwa." aliongezea

Moja kati ya vijana  aliyepatiwa mafunzo na chama cha uwandishi wa habari wanawake  TAMWA -Zanzibar ,Maimuna Kassimu Yussuf amesema baada ya kupewa mafunzo na chama hicho alifanikiwa kupata nafasi mbalimbali za uwongozi .

" Elimu niliyoipata kutoka tamwa imenisaidia kushika nafasi mbalimbali ikiwemo kuwa mjumbe katika chama cha mpira wa miguu wilaya ya kati,"alisema

"nikaendelea kupambana tena katika kamati ya uchaguzi wa kamati ya maendeleo shehia ya kowani nikafanikiwa kuwa mjumbe wa pili. " alisema

Pia amewasaa vijana wenzake kuendelea kupambana kugombania nafasi za uwongozi kwa lengo la kujinua kiuchumi.

Lakini licha ya yote hayo kuna mtazamo kwamba mwanamke hawezi kuwa kiongozi kwa misingi ya dini ya kiislamu na hivyo kuwafanya baadhi ya wanawake washindwe Kwenda kwenye majimbo na kugombea.

Amina Salum Khalifan ni kiongozi wa dini je anazungumziaje suala hilo?.

"Hakuna dini yoyote iliyokataza mwanamke kuwa kiongonzi tukiangalia katika enzi za Mtume Muhamma (SAW) tunaambiwa kuwa sio tu alishirikiana na wanawake katika uongozi, bali  aliwapa nafasi ya kuongoza, hata katika mapigano ya kusimamisha dini ya Kiislamu." alisema

Sambamba na hayo alisema kuna miongoni mwa wanawake walio shikilia nyadhifa za umma au nyadhifa  kubwa katika karne ya mwanzo na ya pili Hijria, na kushirikiana na mtume.

"Mwanamke wa mwanzo aliyeshika na kukubaliwa wadhifa wa ushauri kwa Mtume (SAW) alikuwa mama yetu mkubwa, Sayyidatuna Khadija binti Khuwayld (Radhiya llahu Anhu) ambaye alikuwa mshauri wake mkuu kwa hali na mali hata siku moja, Mtume (SAW) hakuwahi kuukataa ushauri wake." alisema

Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Shukuru Malonda, alisema mwanamke ana nafasi ya uongozi katika kanisa na kijamii na kutoa mfano wa viongozi wa kike.

 Pia amesema waliongoza na kuwasimamia watu katika dini ya Kikirsto.Miongoni mwao ni Esta ambae alikuwa Malkia na Debora alikuwa Nabii.

"Katika kanisa letu tumewachaguwa wanawake wawili   na wanaume wanne ambao  ni wachungaji na Wainjilist 12,  wanawake watano na wanaume saba, ndio wanaoongoza kanisa," alisema.

Mkurugenzi wa Uchaguzi Zanzibar ( ZEC), Thabit Idarous Faina amesema hali halisi ya viongozi wanawake Zanzibar kupitia nafasi ya uwakilishi kwenye majimbo 50 ya Zanzibar ni idadi ya mawaziri sita katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, sawa na asilimia 33, makatibu wakuu ni saba ambayo ni sawa na asilimia 39.

Kuhusu wakuu wa mikoa, alisema yupo mwanamke mmoja tu, ikiwa ni sawa na asilimia 20 ,wakuu wa wilaya wapo wanane ambayo ni sawa na asilimia 36 na Masheha 389 waliopo nchi nzima, 68 tu ndio wanawake ambayo ni asilimia 17.

Katika mwaka 1964 wabunge wanawake  walikuwa 3 hadi sasa wabunge wanawake wako 148 sawa asilimia 37.7 ya wabunge wote 390 walioko sasa.

Leo hii kati ya mihimili mitatu ya dola,wanawake wanaongoza mihimili  miwili, Serikali na bunge jambo linalothibitisha kuendelea kuimarika kwa usawa na kijinsia.

Post a Comment

0 Comments