DKt. Samia Suluhu Hassan Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania |
Na Ahmed Abdulla:
Katika miaka ya karibu
asasi nyingi za kiraia ziliopo Zanzibar zimeongeza nguvu katika kujenga
mazingira ya kuwa na usawa wa kijinsia kwenye nafasi za uongozi.
Lengo ni kuona nafasi hizi
zinashikiliwa bila ya vikwazo wa aina yoyote ule wa kijinsia ili kuimarisha
mfumo wa utawala wa demokrasia.
Nguvu hizi zitakuwa na
tija kama patakuwepo matokeo yatakayoleta mabadiliko kwenye jamii.
Katika harakati hizi zipo
jumuiya ambazo unaweza kusema zimekuwa mstari wa mbele kwenye kutoa elimu
juu ya suala hili na kuwa mstari wa mbeke katika utetezi wa wanawake, kuanzia
akiwa mtoto hadi mtu mzima.
Miongoni mwao ni Chama Cha
waandishi wa Habari Wanawake TAMWA-Zanzibar ambayo imekuwa ikifanya juhudi za
kuhakikisha wanawake wanapata nafasi za viongozi, kama ilivyo kwa wanaume.
Mkurugenzi wa
TAMWA-Zanzbar, Dk. Mzuri Issa, akiiambia Zanlight blog kuwa kumalizikwa hivi
karibuni kwa mradi wa kuwawezesha wanawake kwenye kushika nafasi za uongozi
isiwe sababu ya kuzuia harakati hizo ziendelee.
Badala yake iwe hatua ya
kwanza ya safari ya kuhakikisha wanawake wanapata haki yao ya kushiriki katika
kuiongoza jamii na nchi kwa ujumla.
“Sasa ni wakati wa
kuendeleza kampeni kwa kutoa habari zinazohusu wanawake ili kuleta
uchechemuzi wa kufikia lengo kuu la kuwa na usawa wa kijinsia kwenye
nafasi za uongozi”, alieleza
Alisema mradi wa viungo
unaoendeshwa na jumuiya yake na ule wa kijaluba pia unasaidia unachochea nguvu
ya mwanamke, hasa katika eneo la kiuchumi.
Aliwataka wale
walionufaika na miradi hiyo ifikapo mwaka 2025 wajitahidi kuleta
matokeo chanya kwenye uchaguzi mkuu.
Jukwaa la Walimu Wanawake
wa Kiafrika (FAWE) upande wa Zanzibar nalo ni shirika linalojipambanua kwa
kuwawezesha wanawake kiuchumi na kielimu.
Mpango wake wa kuwawezesha
wanawake kwenye uongozi umelenga zaidi katika elimu na uchumi ikiwa kwa
kuwapatia wanawake mafunzo na mitaji ya kuendesha shughuli mbali mbali.
Mkurugenzi wa Shirika hilo
kwa Zanzibar, Winnifred Yatuwa Mamawi, alisema lengo ni kuhakikisha
mwanamke anasimama mwenyewe kusaka nafasi za uonguzi.
“Tumewaingiza watetezi wa
masuala ya jinsia wanawake na wanaume kwa sababu wanaume ndio wamekuwa kikwazo
kikubwa cha wanawake kusoga mbele kupata nafasi za uongozi”, alisema
Miongoni mwa hatua
ziliochukuliwa na FAWE ni kutoa mitaji ya Shilingi millioni tatu na sasa
kiwango kimeongezwa na kuwa milioni 10.
Lengo ni kuendelea na
mradi huo na mtaji kufikia zaidi ya milioni 20 ifikapo mwaka 2025.
“Tunatarajia ifikapo mwaka
2025 wanawake wawe wanaweza kuendesha biashara zao wenyewe na wengine
kujisimamia katika kusaka uongozi”, aliongeza
Taasis nyengine inayofanya
kazi hii ni Community Forest Pemba inayojikita katika kumuwezesha mwanamke kwa
njia tatu zinazolenga kumuimarisha kiuchumi.
Hii itamuwezesha kukweka
malengo yake pasina kuwepo kwa changamoto ziliopo hivi sasa.
Mkurugenzi wa jumuiya
hiyo, Mbarouk Mussa Omar, aliieleza Blog kuwa katika mradi wao wa kuwawezesha
wanawake kukabiliana na hali za kiuchumi wamelenga kuwfikia wanawake 400 katika
kuwaandaa kuwa viongozi.
“Kwa ujumla tumelenga
kuwafikia wanawake 4,000, katika hao tunakitaji wanawake 1,800 tuwapeleke
kwenye uhifadhi wa misitu, 1,200 kwenye mikoko, 600 kwenye masuala ya
Jinsia na wengine 400 watakwenda kwenye masuala ya uongozi.
Matarajio ya nguvu hizi
Rais wa Tanzania, Dkt.
Samia Suluhu Hassan, amekuwa akiwataka wanawake kujitokeza kwa wingi
kugombea uongozi, sambamba na walioteuliwa waonyeshe uwezo na uadilifu mkubwa.
Ni dhahiri kuwa
inawezekana kwa Zanzibar kufikia mgao wa nafasi za uongozi kati ya wanaume na
wanawake kufikia asilimia 50 kwa 50.
Lakini hili linahitaji
kufanyiwa kazi na zaidi na wanawake, kwanza kwa kujiamini na kujitokeza kuwania
nafasi za uongozi.
Vile vile upo muhimu wa
kuwabadilisha mitazamo wanaume wanaodhani mwanamke hawezi kuongoza.
0 Comments