Na Ahmed Abdulla, Zanzibar:
Mkurugunzi wa Chama cha Waandishi wa habari wanawake Dk
Mzuri Issa amewataka wanawake nchini kujiamini na kuondokana na woga wakati wa
kugombea nafasi za Uongozi kwa lengo la kuleta mabadiliko katika jamii.
Dk Mzuri ameyasema hayo wakati wa mkutano uliowashirikisha
wasomi wanawake kutoka vyuo vikuu tofauti wakipata mafunzo juu ya kugombea
nafasi za Uongozi uliofanyika katika Ofisi za
TAMWA ZNZ , Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.
Amesema kwa sasa dunia imetambuwa umuhimu wa mwanamke na imeamini
mwanamke ni Kiongozi kutokana na utofauti uliopo kati yake na mwanamme kwa kuwa
na uwezo wa kufanya kazi nyingi kwa wakati mmoja huku akitekeleza majukumu yake
ipasavyo.
“Mwanamke anaweza kuwa mama, mke, mfanyakazi na Kiongoz na
wakati huo huo akitekeleza majukumu yote
hayo kwa wakati mmoja na akafanya vizuri
katika kila sekta bila kuathiri upande wowote kama wengine wanavyodhani, Dk
Mzuri Issa , Mkurugenzi TAMWA ZNZ.
Akitowa mafunzo hayo kwa wanawake wasomi Mshauri Elekezi Inilda
Lulu Orio amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwasaidia kuwajengea uwezo wa
kujitambuwa na nakutambuwa nafasi zao ili kufikia ndoto zao katika harakati za
Uongozi.
“Nafasi ya wanawake kwa sasa inazidi kuongezeka kwa sababu
kuna ukuwaji wa Elimu kwa jamii na hata watoto wakike wenyewe kwa sababu
Uongozi unajengwa , tumeona baadhi ya jamii inavyowajenga watoto wa kike kuweza
kujitambuwa na Ongezeko kubwa la Viongozi wanawake, Inilda Lulu Orio, Mshauri
Elekezi.
Nae Mratibu wa mradi wa kuwawezesha wanawake kugombea nafasi
za Uongozi (SWIL) Maryam Ame Chuom amesema kwa mda mrefu imeonekana wanawake
wameachwa nyuma katika ngazi za maamuzi hivyo kwa sasa wanawake watumie fursa
na haki yao ya kikatiba ya kuchaguwa na kuchaguliwa.
Aidha washiriki wa mafunzo hayo wamesema wamefarajika kupata
mafunzo hayo na watakuwa mabalozi wazuri kwa wanawake na kupambana kugombania
nafasi za ngazi za juu ili kuondosha mfumo dume uliotawala katika jamii.
“Matarajio yangu baada ya mafunzo haya ni kuwa Kiongozi
mwenye kujiamini, mimi ni kiongozi , na baadaa ya hapo nitapambana kuwa
kiongozi wa nagazi ya juu zaidi katika chuo change, Hudhaimat Haji Juma,
Mwanafunzi wa Shahada ya Pili ya Uhasibu katika Chuo Kikuu cha Taifa, Campus ya
Chwaka.
Mradi wa kuwajengea uwezo wanawake kugombea nafasi za
Uongozi unaotekelezwa kwa pamoja na TAMWA ZNZ, PEGAO NA ZAFELA umewashirikisha
wanawake kumi na tano kutoka vyuo Vikuu chini ya ufadhili ya NORWAY.
0 Comments