Ticker

6/recent/ticker-posts

Wananchi Wa Shehia Ya Kidagoni, Kaskazini “A” Wakosa Haki Yao Ya Msingi Ya Elimu Kutokana Na Umbali Wa SkuliNa Ahmed Abdulla, Zanzibar

Wakati dunia ikiwa inapambana na usawa wa kijinsia kati ya wanawake na wanaume katika kupata huduma mbalimbali lakini bado sekta ya elimu kwenye baadhi ya maeneo Visiwani Zanzibar imekuwa ni changamoto kupatikana kwake.

Miongoni mwa maeneo yenye changamoto hiyo ni pamoja na kigongoni, Bwereu na kidoti na hii ni kutokana na umbali wa skuli jambo ambalo hisababisha kwa siku wanafunzi zaidi ya 30 kutoka maeneo hayo kushindwa kuhudhuria skuli.

Wakati idadi hiyo ikiwa ni ya siku lakini kwa mwaka nzima ambao siku za kati ni wastani wa siku kazi ni 240 basi ni wanafunzi 7,200 wanakosa huduma hiyo muhimu.

Kama tunavyofahamu elimu ni msingi wa yote hii inaashiria kuwa lile lengo la baadhi ya jumuiya zisizo za kiserikali ikiwemo TAMWA Zanzibar, mashirika yanayopigania asilimia 50 kwa 50 ya nafasi za wanawake kwenye uongozi pamoja na serikali yenyewe kupuitia kwa sera ya jinsia la kupigania usawa wa kijinsia hasa kwenye Demokrasia na uongozi litakuwa halifikiwi.

Tunazungumza halifikiwi kwa sababu katika 7,200 wamo watoto wakike ambao ndio tunalenga wafikie lengo hilo lakini pia katika idadi hiyo tunategemea kupata wataalamu bora yatakaleta mabadiliko kwenye masuala hayo jee kwa msingi huo lengo litafikiwa? Ni kwamba haliwezi kufikiwa.

Tulipomuuliza mwalimu mkuu wa skuli ya maandalizi na msingi Kidagoni Machano Khamis Machano  sababu zinazopelekea idadi hiyo kushinda kuhudhuria masomo yao tukitoa umbali wa skuli alisema “wanafunzi wanatoka majumbani kwao lakini hawafiki skuli, kuna kijiji kinaitwa Kijini Mbumbwi ni sehemu ambayo iko mbali, watoto wengi wanatoka huko tena wadogo wa Maandalizi na ni pori tupu, mwendo wa saa moja huko hakuna skuli kwa hiyo wanakosa haki yao ya msingi ya kupata Elimu.”

Alisema wanafunzi wanaosoma katika skuli hiyo wanatoka shehia ya kigongoni, Bwereu na kidoti ambapo kutoka maeneo hayo hadi kufika skuli ni Zaidi ya saa moja kutembea huku njia zenyewe zikiwa haziridhishi kwasababu hatarishi.

Wazazi wa watoto hao wliesema kwa sasa Watoto  wanasoma skuli ya  mbali ambayo wanatembea Zaidi ya saa moja hali inayohatarisha usalama wao na wengine kushindwa  kufika skuli kuendelea na masoma na kuishia vichakani .

“Skuli iko mbali na sisi inabidi twende Fukuchani. Kidagoni au Kidoti hali ambayo ina hatarisha usalama wa watoto wetu, na sisi wazazi huwa hatuna Amani mpaka watoto warudi skuli,” Mwananchi, Shehia ya Kidagoni.

Mmoja wa wananchi hao Ali Simai Silima alisema shehia hiyo ya kigongoni hakuna skuli na badala yake Watoto wa eneo hilo wanakwenda kusoma skuli ya kidagoni ambayo ni mbali na shehia hiyo.

“Vijana wangu wanasoma maeneo ya mbali tumejenga banda la skuli katika maeneo ya karibu lakini baadhi ya Viongozi wa chini  wametwambia tuondoshe baadhi wanafunzi hasa watoto wadogo wamekata kwenda skuli kabisa kutokana na masafa ya mbali,” Mwananchi. Alisema Mwananchi huyo

Aidha aliongeza kuwa Watoto wake kusoma kwa umbali huo anakosa amani kutokana na dunia kukumbwa na matukio mengi ya kihalifu ikiwemo udhalilishaji.

“Mtoto akitoka kwenda skuli hafiki anakwama njiani,unaambiwa wende ukachukuwe mwanao, tunawaambia Viongozi wetu wa Jimbo kama wanatutaka mwakani tuwapigie kura walitazame suala hili kwa umakini, sisi wazee ndio tunaoumia. Alisema kwa msisitizo

Mwalimu wa skuli hiyo Zainab Silima Machano aliiomba serikali kuwawekea miundombinu mizuri ambayo itasaidia kufika skuli hapo kwa wakati kwasababu anatoka masafa marefu na akifika skuli huwa kashachoka na kusababisha kushindwa kuvikosa baadhi ya vipindi hususani vya asubuhi.

“Tunatoka mbali na changamoto hamna usafiri, watoto wanachelewa na pia wanakuwa watoro na kama kipindi chako ni cha kwanza hata ukifika skuli kushakikosa kwa kuchelewa,” Mwalim wa Skuli ya Kidagoni Zainab Silima Machano.

Baadhi ya wanafunzi wa skuli hiyo walisema hali hiyo ya umbali wa skuli inawaathiri hasa kwenye masomo yao ambapo muda mwingi wanautumia njiani badala ya kusoma hivyo wameiomba serikali kuwajengea skuli ya karibu ili kupata haki yao ya elimu bila ya usumbufu.

“Tukifika skuli tumechoka tokea kiwiliwili mpaka akili na masomo mengi tunakosa kutokana na kutembea masafa marefu, hivyo tunaomba Serikali itusaidie,” Mwanafunzi kutoka skuli ya Kidagoni.

Akizungumzia tatizo hilo Sheha wa shehia hiyo Vuai Mtosho Bure alisema hatua aliochukua ni kushirikiana na wananchi wake kuanza ujenzi wa skuli ya maandalizi katika maeneo hayo ya karibu ili kuwaondoshea usumbufu watoto wadogo kufuata huduma hiyo katika masafa ya mbali.

“Naiomba  Serikali  kuu na wadau wengine wa maendeleo kuwakamilishia ujenzi wa skuli yao kwani wamekwenda katika maeneo mbalimbali ikiwemo uongozi wa Jimbo na halmashauri lakini bado hawajafanikiwa,” Sheha Kidagoni, Vuai Mtosho Bure.

Mratibu wa mradi wa kuwainua wanawake katika uongozi SWIL kutoka chama cha waandishi wa Habari wanawake Tanzania TAMWA Zanzibar Mariam Ame Chum alisema  wanafanya ziara za mara kwa mara katika vijiji lengo ikiwa ni kuibua changamoto zinazoikabili jamii ili ziwe kufanyiwa kazi na wananchi waweze kupata huduma bora ambazo ni haki yao ya msingi, ikiwemo elimu , mali na miundombinu ya Barabara.

“Viongozi wa majimbo waliochaguliwa na wanachi watimize wajibu wao ipasavyo kuwahudumia wananchi na kupata haki zao za kidemokrasia kwa kutatuwa changamoto mbali mbali zinazowakabili kupitia majimbo yao,”Mariam Ame Choum. Mratibu SWIL,TAMWA,ZNZ. 

Wakati Sera ya Elimu ya Zanzibar (1991), Ngazi ya Maandalizi inasema inawakusudia watoto wa miaka minne mpaka sita (4-6) 

Aidha Sera hii inaeleza kwamba Vituo vya kutoa elimu hii vitaenezwa kwa mujibu wa haja na uwezo utakavyoruhusu kwa masharti yatakayowekwa. 

Kupitia changamoto hiyo na lengo linalohitaji kufikiwa mamlaka zinatakiwa kufanya kazi kwa bidii usiku na mchana ili kuona viongozi hawa wa baadae wanapata huduma ya elimu katika mazingira mazuri na salama.

Tamwa Zanzibar inatekeleza mradi huo wa kuwainua wanawake katika uongozi sambamba na kuibu changamoto za wananchi na kuwawezesha kupaza sauti zao kwa kudai haki zao za msingi kwa kushirikiana na ZAFELA na PEGAO chini ya ufadhili wa ubalozi wa Norway.

Post a Comment

0 Comments