Ticker

6/recent/ticker-posts

-Marta Kinara wa Mabao Kombe La Dunia



Na Theresia Severini:

Kombe la dunia kwa upande wa wanawake 2023 litatukumbusha kwamba kuna mwanasoka wa kike mashuhuri zaidi katika kombe la dunia kwenye swala zima la ufungaji ambaye ni Marta Vieira Da Silva.


Marta 37,anatajwa kuwa ndie mfungaji bora kwa sasa wa kombe la dunia akiwa na magoli 17 na si kwa upande wa wanawake tu bali hata kwa upande wa wanaume kwani amempita Mjerumani Miroslav Klose mwenye magoli 16 ambae ndie mfungaji kinara kwa upande wa wanaume.



Mwanamama huyu anaekipiga Orlando Pride ya Marekani ana rekodi mbalimbali kwenye soka ikiwemo Jumla ya ushiriki 6 wa Kombe la Dunia la FIFA la Wanawake, Mchezaji wa kwanza kufunga katika matoleo 5 ya Kombe la Dunia, Mshindi wa Mpira wa Dhahabu na Kiatu Dhahabu cha Kombe la Dunia la Wanawake la FIFA 2007.

Licha ya hayo maisha ya Marta kwenye Kombe la Dunia la Wanawake yanaonekana kufikia kikomo mara baada ya Brazil kuondolewa katika mchuano ya mwaka huu na Jamaica .

Huyu ndiye Marta Queen Anejua kucheka na nyavu za wapinzani.


Post a Comment

0 Comments