Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Ussi Salum Pondeza akimkabidhi mmoja wa wananchi wa Jimbo hilo mfuko wenye vyakula mbalimbali pamoja na bahasha yenye fedha taslim
Jumla ya watu 854 wa jimbo la Chumbuni
wamefikiwa sadaka ya vyakula inayotolewa na mbunge wa jimbo hilo Ussi Salum
Pondeza kwa mfungo huu wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Idadi hiyo ni sawa na asilimia 51.14 ya walengwa
wote 1670 watakaofikiwa katika kipindi kizima cha mfungo huo.
Akizungumza mara baada ya zoezi la kugawa sadaka
kwa kaya maskini za shehia sita za Jimbo la Chumbuni, mbunge wa jimbo hilo Ussi
Salum Pondeza alisema azma yake ni kuona wananchi wake wanakuwa na uhakika wa
futari katika mfungo huo.
“nimejiwekea kila mwezi mtukufu wa Ramadhani
niwe natoa sadaka kwenye jimbo langu nan je ya jimbo langu” alisema Pondeza
Alisema kwa leo amewafikia watu wenye hali duni
ya kiuchumi ili awapatie sadaka hiyo hali itakayowawezesha kumufu futari ndani
ya siku kadhaa.
“Tumewatafuta ambao hawako vizuri kiuchumi ili
tuwapatie sadaka hiyo iwasaidie kwa siku chache. Aliongezea Mbunge huyo
Kwa upande wa wananchi waliopatiwa sadaka hiyo
walimpongeza mbunge huyo kwa kuwajali na kuwathamini katika kipindi hiki cha
mfungo huku wakiwaomba viongozi wengine kufuata nyayo za mbunge huyo.
“mbunge anatusaidia sada kwa mfano leo ingekuwa
sina futari hii ingetusaidia” alisema mmoja wa wananchi
Mbali na zoezi hilo mbunge huyo pia aliwapatia
sadaka ya fedha watoto wa jimbo hilo.
Mbunge wa Jimbo La Chumbuni Ussi Salum Pondeza akimkabidhi Mtoto wa jimbo hilo sadaka ya Fedha Taslim |
0 Comments