Na Ahmed Abdullah
Kwa sasa siajabu tena ukifika mjini Unguja majira ya mchana na
jioni kukutana na watu wenye ulemavu wanaofanya kazi ya kuomba watu pesa na
kuna wakati wameanza kuwa kero na mara kadhaa wamewahi kurudishwa wanapoishi.
Makala ya uchunguzi imebaini kuwa uwepo wa watu hao ambao kikawaida huletwa na gari maalumu kila ifikapo asubuhi na kugawiwa maeneo maalumu ya
kuwekwa kwa mchana kutwa huku wakiendelea na kazi hiyo.
Mila na desturi za kizanzibar hazikuwahi kushuhudia tabia hiyo
ambayo kwa kiasia kikubwa inachafua taaswira ya watu wenye ulemavu kiujumla.
Inaaminika kuwa kuna watu maalumu walioamua kuwageuza watu wenye
ulemavu kama sehemu ya mtaji kwenye maisha yao na ndio maana inasemakana
huwakodia hadi nyumba na kuwaweka pamoja.
Kwa mujibu wa sheria namba 9 ya mwaka 2006 Wajibu wa kulinda haki
za watu wenye ulemavu (20)Watu wenye ulemavu hawatabaguliwa na kudhalilishwa
kwa namna yoyote ile na katika ngazi yoyote na katika ngazi zozote zile
kutokana na sababu ya ulemavu.
Swali ambalo tunaweza kujiuliza ni kwanini watu wenye ulemavu
hukubali kuwa mtaji wa biashara hii?
Kwa uchunguzi wa ndani kabisa unabaini baadhi ya watu wenye
ulemavu wamekua wakiathirika kisaikolojia kwa kukosa kwao watu muhimu kwenye
mfumo mzima wa maisha yao ambao wangewasemesha na kuwajenga kinadharia ili
waweze kufanya shughuli mbali mbali za kujingizia kipato.
Kukosa kwao nadharia hii muhimu ya stadi za maisha imekua
ikiwakosesha uwezo wa kufikiri watu hawa na kuamini kuwa wao si sehemu ya jamii
wanayoweza kufanya lolote lile bali wanastahiki kuomba na kupatiwa fedha kitu
ambacho kubadilikwa inawezekana.
Katibu mtendaji wa Baraza la watu wenye ulemavu Zanzibar Ussi
Khamis anasema kuna tatizo la baadhi ya watu wenye ulemavu kukosa ukaribu na
watu muhimu kwenye maisha yao.
Alisema watu wenye ulemavu huzaliwa wakiwa pungufu hivyo hujiona
si sehemu wanayo stahiki kufanya lolote lile bali wanahitahi msaada tu,na
kwamba mtazamo huo unahitaji kubadilishwa.
Alisema tabia ya omba omba inaanzia tokea wakiwa na umri mdogo kwa
sababu ya kukosa misingi ya utaftaji na ndio maana huwa warahisi
wanaposhawishiwa na watu wenye nia ovu.
Kwa masharti ya kutotajwa jina mmoja ambae alikua mkaazi wa karibu
na nyumba waliopangiwa au waliopanga wenye mjini Unguja alisema ilikua kawaida
kila siku ifikapo saa 12 za asubuhi kuiona gari maalumu iliokua inakuja na
kuwachukua kwenye nyumba hio watu hao na badae huwarejesha jioni.
Alisema utaratibu huo ulimfanya yeye kushangazwa na kutaka kujua
haswa ni nani wanaofanya alichokiita na kudhani biashara na ndipo walipo
taarifu uongozi wa shehia na hatua zilianza kuchukuliwa.
Wasemavyo wahusika.
Kwa mazingira magumu mmoja ya watu wenye ulemavu alikuabali
kuzungumza na mwandishi wa habari hii bila ya kujua kuwa ni mwandishi na
kumuelewa kuwa wanaweza kukusanya hadi elfu hamsini baadhi ya siku na inaweza
kwenda hivyo hadi wiki nzima.
Alisema kuna watu ambao wanawapelekea pesa hizo na badae hufanyika
mgao na wahusika ukizingatia wana mahitaji ambayo hupatiwa kila leo hivyo
wanalazimika kuwa sehemu ya wanaochangia huduma hizo.
Msimamo wa Serikali.
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa mara kadhaa imewahi kuzungumzia
jambo hilo nma kuonesha kukerwa kwake na kusema haipo tayari kuona watu wenye
ulemavu kuheuka kuwa omba omba.
Kauli ya TAMWA-ZNZ
Mkurugenzi wa Chama cha waandishi wa habari wanawake TAMWA-ZNZ
Dkt,Mzuri Issa alisema ulemavu usiwe sababu ya wahusika kutofanya kazi bali
wanapaswa kujitambua kuwa ni sehemu ya maumbile ambayo wamejaaliwa.
Pamoja na hayo aliwataka waandishi wa habari kujikita zaidi
kuandika habari zinazohusu watu wenye ulemavu na harakati zao huku lengo kubwa
likiwa ni kuwasaidia kwa hali na mali.
0 Comments