Ticker

6/recent/ticker-posts

Sekta ya ajira isibague watu wenye ulemavu Z'bar

 

Sehemu ya vigari vya watu wenye ulemavu,vilivyobeba taaswira ya tukio husika.Picha kwa hisani ya mtandao.

Na Ahmed Abdulla

Katika hali isiokua ya kawaida visiwani Zanzibar si ajabu kukuta watu wenye ulemavu wakiendelea kulalamikia ubaguzi na ukandamizwaji wa haki na usawa katika sekta ya ajira ktokana na mapungufu waliojaliwa na muumba.

Kwa masharti ya kutotajwa jina mmoja miongoni mwa mt mwenye ulemavu alimuambia mwandishi wa habari hizi zaidi ya mara mbili amewahi kuomba nafasi ya kazi katika taasisi binafsi lakini hakuwahi hata kuitwa kwenye usaili (interview)

Alisema yeye ni msomi mwenye diploma ya alimu ambayo anaamini kuwa ni mwenye uwezo wa kusomesha kwa madarasa ya msingi na hata ya awali lakini amekua akikosa nafasi ya kazi kwa sababu anachokiamini ni kutokana na ulemavu wake alionao.

Anaseam anachokifaham kuwa katiba ya Zanzibar na hata hile ya Jamuhuri ya Muungano Tanzania imeweka wazi kuwa binadamu wote ni sawa na wastahiki haki sawa bila ubaguzi wowote hule.

Pamoja na matakwa hayo ya katiba lakini pia haki hiyo imeongezewa nguvu na Sheria ya watu wenye ulemavu Zanzibar ya mwaka 2022 ambayo katika moja ya kipengele cha sheria hiyo kimeleza wazi na kufafanua.

‘’Kwa kuzingatia masharti ya kifungu kidogo cha (1) (b) cha kifungu hiki taasisi yoyote zenye dhamana ya kazi za utumishi wa umma  zitahakikisha kuwa zinatoa kipao mbele na mazingatio kwa nafazi za ajira zinazotolewa katika sekta ua umma na sekta binafsi kwa wat wenye ulemavu’’

Licha ya uwepo wa misingi hii miwili ya katiba na sheria ya watu wenye ulemavu hadi sasa bado baadhi ya watendaji kwenye taasisi wameshindwa kuiheshimu na bado wanaendeleza ubaguzi kwenye sekta ya ajira.

Uchunguzi wa ndani wa mwandishi wa habari hizi umethibitisha kuwa watu wenye nafasi za kutoa ajira wamekua na mtazamo potofu ambao miongoni mwao hawaamini kama kutoa nafasi kwa watu wenye ulemavu wanaweza kufanya kazi.

Athari za ubaguzi huu ni zipi?

Ndiolo swali ambalo wengi wanaendelea kujiuliza kila leo kwa sabbabu yanagonga vichwa.

Mtaalamu wa maswala ya utafiti kutoka chuo kikuu cha Zanzibar University Hafidh Ali alisema kuendelea kuwabagua watu wenye ulemavu katika sekta ya ajira ni kunyima haki yao muhimu.

Alisema ubaguzi huo unawaathiri pia kisaikolojia na kupelekea wengi wao kukata tamaa na kubaki wakiendelea kubaki kuwa watu wenye mawazo kwa muda wote.

‘’Unaja tulipo sasa tofauti na miaka ya nyuma hivi sasa watu wenye ulemavu wanasoma na wana uelewa mkubwa wa kufanya kazi kuliko ilivyokua miaka ya nyuma’’alisisitiza.

Post a Comment

0 Comments