Ticker

6/recent/ticker-posts

KWANINI GUARDIOLA ALIMUITA ARTETA UINGEREZA?

 


IMEANDIKWA NA SWALEH SHRIMP:


Mikel Arteta alikutana Josep Sala akiwa na  umri wa miaka 15 huko Catalunya na Uhispania Kati yao ulianza kujengwa huko muda ukapita Mikel alitangulia Uingereza akiwa  Mchezaji huku Guardiol yeye alibaki Uhispania.


Pep Guardiola Wakati anamalizia maisha pale Ujerumani  aliwasiliana na Arteta ambaye kwa wakati huo alikuwa yupo Uingereza na kumuelezea Kama ana  ndoto ya kufanya kile alichokifanya akiwa  Barcelona kwenye ligi aje kukifanya Uingereza .


Guardiol alimwambia Arteta  "Nafahamu Kama unaona  ni ngumu na haiwezekani hata wengeni wanahisi Hivyo Lakini nakuomba uje kuwa  msaidizi wangu  ili kunisaidia kufikia ndoto hiyo".

Pep Guardiol alipotuwa Manchester City mnamo mwaka  2016, alimwambia Sheikh Mansour Kama anamuhitaji Arteta kando yake ili Safari yake isiwe ngumu.


Hapo Mikel Arteta alikuwa amemaliza  maisha yake ya uchezaji akiwa na Arsenal, na alikuwa na fursa ya kufanya kazi katika akademi yao,  lakini aliamua kumfata Guardiol licha ya kuwa na mashaka kuhusu kuchukua kazi kubwa kama jukumu lake la kwanza katika ukocha.


Arteta alipofika Manchester City alimwambia Guardiol "Sijafundisha mtu yeyote kwa hivyo nitawezaje kuwa  Mkufunzi bora zaidi ulimwenguni na kurudisha kitu ambacho unatarajia nifanye?" ndio hapo Pep alimtizama usoni Mikel huku  akitabasamu na  kumjibu "Nilikuwa nakuhitaji wewe na sio  wasiwasi wako hivyo umefika nakushukuru".


Safari ikaanza Pep Guardiol akawa ana kazi mbili akimaliza kuifundisha timu anamchukuwa Mikel Arteta na kuanza kumpa darasa na kesho yake Arteta akawa anafunguwa yeye zoezi la timu. 


Guardiol alimwambia Arteta  kwamba apendelee kusikilizi Sana kwa umakini  hii itapelekea kuongea kidogo na kufahamika na hapo  wachezaji wa City  walikuwa wepesi  kumuelewa Mikel akianza kufunguwa zoezi na ikazidisha imani kati yao.


Licha ya Mwaka wa kwanza wa Pep kwenda kinyume na mpango kwani City ambayo ilimaliza msimu wa 2016-17 bila taji lolote lakini Imani ya Guardiol kwa Arteta  haikuyumba kwasababu alikuwa na imani Kwamba  timu inaelekea katika mwelekeo sahihi.


Arteta alimwambia Pep Guardiol kuwa  "Ni muda Sasa wa  kuelewa utamaduni wa soka la Uingereza jinsi waamuzi wanavyofanya, jinsi vyombo vya habari vinavyofanya kazi" Basi Walikaa chini na mafaili yote na kilichofata ni HISTORIA tu .

Post a Comment

0 Comments