Ticker

6/recent/ticker-posts

Yanayokwamisha wanawake wa Z'bar kutoshika nafasi za uongozi

 

Baadhi ya wanachama wa Chama cha Wananchi CUF wakiwa kwenye mkutano wa hadhara katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015  ambapo wengi wa waliohudhuria katika mkutano huo ni wanawake.Picha kwa Hisani mtandao 


Na Ahmed Abdalla


Wakati Dunia ikiendelea kupaza sauti juu ya ushiriki wa wanawake katika nafasi mbali mbali za uongozi Zanzibar nayo haipo nyuma  katika harakati hizo kupitia chama cha Waaandishi wa habari wanawake Tanzania (TAMWA-ZNZ) na wadau wengine wamekua wakiendelea na harakati za kuwapigania wanawake bila kuchoka, usiku na mchana ili kutumiza ndoto za walio wengi zinazojaribu kukatishwa kila leo na watu wenye dhamira zao binasi zikiwemo za kuwadumaza wanawake na kuendelea kuwafanya ngazi ya kutimiza malengo yao.

Muendelezo wa matakwa haya ya Dunia.Nchini Tanzania ambayo Zanzibar ni sehemu iliyounda Jamuhuri hiyo,inatiliwa mkazo na ibara ya 13.(1) ya katiba ya Tanzania  ambayo   inasema watu wote ni sawa mbele ya sheria na wanayo haki, bila ya ubaguzi wowote, kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria.

 

Kwa msingi huu wa katiba  ni wazi kuwa katiba ya Nchi inatambua haki ya kila mtu kuwa kiongozi hivyo hakuna budi wanawake wengi zaidi kupewa nafasi za uongozi ili kutekeleza haki hii muhimu ya kikatiba.

 

Msingi huu wa katiba unatiliwa mkazo kila leo na wadau mbali mbali ikiwemo TAMWA-ZNZ, katika utekelezaji mradi wa kuwawezesha wanawake kushika nafasi za uongozi (SWIL) ambapo hadi sasa  imefanikiwa kuwafikia wananchi wapatao 8793 kati yao wanawake wakiwa 5276 na wanaume 3217 katika maeneo mbali mbali Unguja na Pemba.

Licha ya kuwa jitihada kubwa zimefanyika lakini nguvu kazi zaidi inahitajika ili kufikia malengo ambayo ni kuleta usawa katika nafasi mbali mbali za uongozi kwa wanaume na wanawake sambamba na ushiriki wa wanawake katika demokrasia.

Itakumbukwa kuwa katika siku za hivi karibuni wakati akitangaza matokeo ya idadi ya sensa ya watu na makaazi Rais wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania Dkt,Samia Suluhu Hassan alisema Zanzibar kama sehemu ya Jamuhuri ya Muungano, ina watu wapatao 1,889,773 kati yao wanaume ni 915,492 sawa na asilimia 48.4 na wanawake ni 974,281 sawa na asilimia 51.6 ambapo licha ya matukio hayo ya  sensa kuonesha kuwepo kwa uongezeko la idadi kubwa ya wanawake kuliko wanaume lakini bado hali halisi ya ushiriki wa wanawake katika uongozi haijaridhisha.

 

Wakati hayo yakijiri kwa upande wa takwimu za tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC) katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi oktoba mwaka 2022 Zanzibar ilikua na idadi ya wapiga kura wapatao 566352 kati, yao wanawake ni 294237 na wanaume ni 272115 pamoja na takwimu hizi pia kuonesha wanawake ndio waliokua wapiga kura wengi zaidi katika uchaguzi huo bado nafasi  nafasi za ushiriki wanawake katika nafasi za uongozi haziendani na uhalisia wa wingi wao jambo ambalo, linawafanya wadau kukosa usingizi kila leo.

Kwa mfano kupitia utafiti  mdogo uliofanywa na mwandishi wa makala haya umebaini kuwa Zanzibar katika majimbo yote  50 ya kupigiwa kura kwa nafasi za uakilishi ni wanawake 8 pekee ndio walipata nafasi ya kuchaguliwa kati ya wanaume 42 na kwa nafasi ya Ubunge kutoka majimbo haya ni wanawake 4 tu ndio walipata nafasi ya kuchaguliwa kati ya wanaume 46.

Huku hayo yakijiri kwa nafasi za ubunge na uakilishi kwa upande wa madiwani Zanzibar ina madiwani 25 wanawake kati ya wanaume 110 na kwa upande wa masheha wanawake ni 64 kati ya wanaume 389 hii, ni wazi kuwa bado jitihada zaidi zinahitajika katika kumkomboa mwanamke.

Je tunakwama wapi?

Ndilo swali ambalo linaendelea kugonga vichwa huku wanaharakati wengi wakiendelea kujiuliza ni wapi haswa Zanzibar inakwama katika kuongeza idadi kubwa ua ushiriki wa wanawake kwenye uongozi na demokrasia.

Wasemavyo wahusika

Halima Ibrahim aliewahi kuwa Mgombea Ubunge Jimbo la Malindi mjini Unguja  kupitia chama cha ACT Wazalendo anasema kuna changamoto mbali mbali ambazo zimekua zikiwakwamisha wanawake wengi wanapotaka kugombea kushika nafasi za uongozi.

Akitaja changamoto hizo alisema ni pamoja na mifumo ya kutoa maamuzi kwenye vyama vya siasa kuwa na idadi kubwa zaidi ya wanaume kuliko wanawake kamati ambazo ndio zenye majukumu ya kuteuwa nani awe mgombea na nani asiwe mgombea.

Alisema kuwepo kwa idadi kubwa ya wanaume ndani ya kamati hizi ni wazi kuwa nafasi ya wanawake haitapewa kipao mbele badala yake wagombea wengi watapitiswwa kuwa wanaume kwani wengi wao hutengeneza urafiki na wajumbe hao.

‘’Kuna wakati hata ukiona mwanamke kapitishwa basi unaweza kumkuta mwanamke kawekwa kwenye jimbo gumu zaidi huku chama chake kikijua kabisa kuwa hawezi kushida na haya ndio yanayotokea kwa mfano utaona majimbo mengi au karibu yote ya Pemba hakukua na mgombea mwanamke’’alifafanua.

Jine Shaame ni mwanachama wa chama cha wananchi CUF aliewahi kuomba ridhaa ya chama chake jimbo la Chonga Wilaya, ya chake chake mkoa wa kusini Pemba alisema aliomba ridhaa ya chama hicho lakini kabla  kujua sababu, madhubuti ambayo ilikifanya chama hicho kuondoa jina lake na kurudisha jina la mgombea mwanaume ambae  anaamini kuwa hakua, sehemu ya mwenye  kukubalika na jamii kuliko yeye na inawezekana ndio sababu ya mgombea wa chama hicho kutoshinda kwenye jimbo hilo.

‘’Hata wazo langu la kuomba ridhaa ya chama changu kuniteuwe lilikuja baada ya kuombwa na wananchi ambao ndio wakaazi wa eneo husika na nilikua na hakika naweza kushinda kwenye jimbo hili lakini sikurudishwa na chama na kupelekea wananchi kununa na kutomchagua alierudishwa na chama changu’’aliongezea.

Kwa masharti ya kutotajwa jina wala chama amabacho aliwahi kuomba alisema wakati anataka kuomba ridhaa alikuatana na changamoto kubwa ambayo ilimkatisha tamaa na kutotamani kuwa kiongozi hata wa nafasi ya chini kwenye chama chake.

Alisema alikumbwa  na mazingira magumu ya kuomba rushwa ya ngono na watu ambao huwezi hata kuamini kwenye vyama vyao kutokana na nafasi walizonazo lakini anashangaa watu kuwaamini na kuona ni watu wema.

Alisema anaamini kuwa kuna viongozi kwenye vyama hawakupaswa kuwa na nafasi hizo kwani wamekua wakizitumia vibaya na kuwapa wakati mgumu wanawake wenye ndoto za kugombea na kuwakomboa wanawake wengi zaidi.

‘’Lazima tukubali ukweli ili wanawake wengi wawe viongozi lazima wavutwe na wanawake wenzao ambao nao pia watakua viongozi ni lazima tupambane na tupambaniwe’’aliongezea.

Pamoja na changamoto hizo zipo pia simulizi zinaeleza  kuwa baadhi ya mitazamo potofu ya dini imekua ikiwafanya wanawake kutokukubalika katika maeneo mbali mbali wakiamini kuwa dini imekua ikikataza wanawake kuwa viongozi hata wa ngazi za awali.

Kauli za viongozi wa dini

Kwa muktadha wa kutaka kujua undani wa mtanzamo huu Sheikh Khamis Abdulatif kutoka mkoa wa kaskazini Unguja anasema hakuna sehemu ambayo dini imekataza mwanamke kuwa kiongozi.

Anasema baadhi ya watu kwenye jamii wamekua wakichukua vipengele vya dini kwa matakwa yao wenyewe lakini uhalisia dini haikukataza mwanamke kuwa kiongozi na kueleza kuwa hata Bwana Mtume Muhammad (S.W) aliwaamuru watu enzi za uhai wake wachote elimu kupitia pia  kwa mke wake Bibi Aisha kuashiria kuwa alikubali na kuwaamini wanawake kama sehemu ya chemchem ya elimu na viongozo.

Kwa upande wake Kiongozi wa dini ya ‘’Chrstian’’ kutoka kanisa la minara miwili Zanzibar Askofu Michael Hafidh alisema kuendelea kuwanyima wanawake fursa za uongozi kwa kisingizio cha dini ni kuwanyima haki zao muhimu ambazo anaamini hakuna dini iliozuia mwanamke kuwa kiongozi.

Wasemavyo wanasiasa

Mwenyekiti wa Chama cha ADC Hamad Rashid Mohamed akifanya mahojiano na mwandishi mwa Makala haya alikiri uwepo wa shida kwenye ushiriki wa wanawake kwenye nafasi za uongozi sambamba na kunasibisha mambo mbali mbali ambayo wenyewe huwa kama sehemu ya tabia zao.

Akitaja miongoni mwa sababu hizo alisema pamoja na ubinafsi unaofanywa na  watu wenye maamuzi ndani ya vyama vya siasa pamoja na  yale anayoyajua yeye  katika historia yake ya siasa ambapo alisema si rahisi kuweza kuyataja hadharani lakini tu alisisitiza jitihada zaidi zinahitajika.

Akizungumza kwa njia ya simu Katibu mkuu chama cha ACT Wazaledo Ado Shaibu alisema chama hicho kimejipambanua kuanzia kwenye katiba ya chama chao kuhusu kuleta usawa katika nafasi za uongozi.

Alisema inawezekana kumekua na changamoto kwenye mamlaka za teuzi na kuahidi kuwa changamoto hizo zitafanyiwa kazi na pia kuongeza ushawishi kwa vyama vyengine vya siasa vitambue umuhimu wa wanawake katika nafasi za uongozi.

Katibu wa itikadi na uendezi chama cha Mapinduzi CCM Katerina Peter Nao alikiri kuwepo kwa changamoto na kusema kuwa licha ya changamoto hizo wanawake wanapaswa kusonga mbele.

Alisema kuna wakati watu wenye nafasi kwa matakwa yao wanaweza kuweka vizingiti vya wengine kusogea mbele lakini wasirudi nyuma na watafute njia mbadala kuona ni kwa namna gani wanaweza kushinda na kutimiza melengo waliojiwekea.

Je wasomi wanasemaje kuhusu hili?

Dkt Yahya Mzee kutoka chuo kikuu cha Zanzibar University,anasema kuna haja ya wanawake wenyewe kujitambua na kujua wanachokitaka,akisema kuwa si ajabu kumuona mgombea mwanamke akishindwa kujua hata vipao mbele vyake kwenye jimbo analoishi na kuwafanya wafuasi kuwa wenye mshangao mkubwa ikiwa mtu anaeomba ridhaa hajui changamto za wananchi wenye jimbo lake.

Alisema wanawake wanapaswa kujengewa uwezo zaidi kwenye siasa na kuzitaka asasi mbali mbali kujikita zaidi ikiwa ni pamoja kuwatengeneza mapema wanawake ambao wana nia ya kugombea, na kuwasisitiza pia kujiongeza kielimu kwani wataongeza upeo na kupambanua mambo mbali mbali ambayo yatawafanya kuwa wabobezi wazuri wa siasa na wajengaji imara wa hoja zenye kukubalika.

Pamoja na hayo alizitaka taasisi mbali mbali zilizojikita kuwasaidia wanawake  kuweka mkakati maalumu wa kuwatambua mapema,wanawake ambao wana nia ya kugombea na kuwajengea uwezo ambao anaamini utawasaidia hata kusimama na kuzungumza mbele za watu jambo ambalo linahitaji ujasiri.

Mtalamu wa maswala ya uchumi ambae pia mi mjumbe katika kamati ya utafiti ya chuo cha Zanzibar University. Hafid Ali aliwashauri wanawake wenye nia ya kutaka kugombea kufanya pia shughuli mbali mbali, za kijasiriamali, kwa lengo la kujingizia kipato na kuweka akiba ili fedha hizo ziweze kuwasaidia wenyewe.

Alisema kwa mazingira yaliopo sasa imefika wakati jamii kuamini zaidi kwenye fedha unapotaka kugombea hivyo wanawake wengi wanashidwa kwa sababu ya kukosa fedha ambazo zingewasaidia hata kuendesha mikutano ya kampeni na mambo mengine.

Mkurugenzi TAMWA-ZNZ atoa ushauri wake

Kwa upande wake Mkurugenzi wa TAMWA-ZNZ Dkt,Mzuri Issa anasema wamekua wakifanya harakati hizo kwa muda mrefu na kwa kiasi fulani wameanza kufahamika kwenye jamii.

Alisema wakati wanaanza harakati za kuwapigania wanawake jamii iliwashangaa sana na kuwaona kama watu wa ajabu wasiojua watendalo lakini leo hii watu wameanza kuelewa ukweli na kuwaunga mkono ingawa kwa asilimia ndogo sana.

Hata hivyo alisema jitihada za pamoja kwa wananchi wote na Asasi za kiraia zinazhitajika kumkomboa, mwanamke katika makucha ambayo yamewafanya kuwa watu  wa kuongozwa na sio wakuongoza, jambo ambalo anaamini kuwa ni kutowafanya wanawake wengi kushindwa kupiga hatua za kimaendeleo.

Akifafanua zaidi alisema pamoja na jitahada mbali mbali za  maendeleo zinazoendelea kufanyika hazitaweza kufanukiwa kwa asilimia mia iwapo ushiriki wa wanawake hautaongezeka na kuwa mkubwa zaiid ikiwezekana kutia kwa falsafa nzima ya hamsini kwa hamsini.

 

                                              Mwisho.

 


Post a Comment

0 Comments