Ticker

6/recent/ticker-posts

TAMWA-ZNZ,Internews Tanzania wawafunda wanahabari Umuhimu wa kujieleza


 


Na Ahmed Abdalla

Imelezwa kuwa haki ya uhuru wa kujieleza ni miongoni mwa haki muhimu katika jamii ambayo ikitekelezwa ipasavyo inachangia kwa kiasi kikubwa kuibadili jamii katika nyanja mbali mbali.

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa miradi kutoka TAMWA-ZNZ Ali Mohamed wakati alipokua akifungua mkutano maalumu wa majadiliano kuhusu umuhimu wa haki ya kujieleza na uhuru wa habari.

Amesema iwapo jamii itajengewa misingi imara ya kutumia haki hiyo ni wazi kuwa kutajengwa jamii bora yenye kuleta usawa kwa kila nyanja.

Alisema kupitia mradi huo unaofanywa na TAMWA-ZNZ kwa mashirikiano na Intaernews Tanzania unalengo la kuwakumbusha wanahabari kuhusu umuhimu wa haki ya kujieleza na kutoa fursa zaidi kwa jamii ili waweze kupaza sauti zao.

Awali wakichangia majadiliano hayo baadhi ya waandishi wa habari walisema kuna changamoto katika upatikanaji wa haki hiyo ukizingatia baadhi ya wanajamii hawafahamu kama ni haki yao ya kikatiba.

Issa Yussuf ambae ni mwakilishi kutoka gazeti la Daylnews alisema licha ya hali hiyo lakini baadhi ya wanahabari nao hawafahamu umuhimu wa haki ya kujieleza na ndio maana wamekua wakiwanyima walio wengi fursa kupitia vyombo vyao vya habari.

Nae Juma Khamis kutoka shirika la magazeti ya Serikali Zanzibar alisema mafanikio yoyote yale kwenye jamii hayawezi kujitokeza pasi na kuwepo kwa uhuru wa habari na kwamba ili tuweze kuendelea ni lazima Nchi iwe na uhuru wa habari wenye kuheshimiwa.

Pia alisema vyombo vya habari vinawajibu wa kutambua kutoa fursa kwa jamii kupaza sauti zao hakuvunji uhuru wala kanuni za habari badala yake ni kuwatendea haki wananchi wasiokua na sauti.

Wakitaja baadhi ya changamoto walisema walisema wanahabari wengi na jamii kwa ujumla wamejawa na hofu na ndio maana hata wao wenyewe hushindwa kuandika au kuripoti baadhi ya habari wanapoona zinawagusa baadhi ya watu.

Sambamba na hayo walisema kutokana na dhana ya hofu iliowajaa wananchi na wanahabari wenyewe wana wajibu wa kuhakikisha kuwa wanajenga jamii huru yenye uwezo wa kusema mapungufu wanayoyaona kila leo.

Kwa upade wake mratibu wa mradi huo Muhammed Khamis alisema mradi huo unatekelezwa na TAMWA-ZNZ kwa kushirikiana na Internews Tanzania wenye lengo la kupitia sheria ya habari  sambamba na kujadili mazingira ya kazi katika tasnia ya habari visiwani Zanzibar.

Alisema kuna umuhimu mkubwa wa watu kupata haki ya kujieleza ukizingatia kuwaweka watu huru huchochea upatikanaji wa maendeleo katioka Taifa lolote ulimwenguni.

Post a Comment

0 Comments