Ticker

6/recent/ticker-posts

Makamu wa kwanza wa Rais Z'bar aguswa na haki ya uhuru wa kujieleza

 


Na Ahmed Abdalla

Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar Othman Massoud Othman amesema sekta ya habari ni miongoni mwa sekta muhimu ambazo zinapaswa kuundiwa sharia bora yenye kukidhi matakwa ya wadau wote kwa maslahi ya Taifa hatimae watu wawe huru kujieleza na kutoa maoni yao.

Aliyasema hivi karibuni wakati wa maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari na kueleza kuwa bila ya uwepo wa sharia borsa ya habari Zanzibar inaweza kuchelewa kuendelea kwa miaka mingi ukizingatia sharia iliopo sasa haiendani na wakati halisi. 

Alisema habari ina mchango mkubwa katika maisha na maendeleo ya mtu, familia, jamii, nchi na mataifa kwa ujumla.

Alieleza kuwa ni dhahiri kuwepo kwa uhuru wa vyombo vya habari ndio kuwepo kwa demokrasia ya kweli katika Nchi, husaidia katika kuimarisha utawala bora, uwazi na uwajibikaji; Wenzetu wanayo mifano mingi katika mwelekeo huo.

‘’Kwa mfano, taarifa zilizochunguzwa na Waandishi wa Habari wa Gazeti la Washington Post la Nchini Marekani, ndizo zilizoibua sakata kubwa linalojulikana kwa jina la Watergate scandal ambalo lilipelekea Rais Richard Nixon kujiuzulu mnamo Mwaka wa 1974, ambapo pia Maafisa wake wa ngazi za juu nao walijiuzulu, huku wengine wakiishia jela.’’alisema.


Alisema uandishi na vyombo vya Habari kwa pamoja, kama vitatumika ipasavyo vitasaidia sana kujenga nchi yenye ufanisi na maendeleo. Hii ni kwa sababu jambo la mwanzo katika kujenga nchi yenye maendeleo ni kuwepo kwa uwajibikaji kwa Serikali, taasisi za umma n ahata za binafsi ambazo zina dhima ya kusimamia mambo ya nchi. Kwa mfano, endapo wanaosimamia shughuli za umma hawatofuata Katiba, Sheria na

Alisema miongoni mwa mambo muhimu katika mazingira rafiki ni uhuru wa vyombo vya Habari. Hivyo, katika siku hii ambayo tunaadhimisha jambo hili muhimu la Uhuru wa Habari, ni vyema kutafakari kwa kiasi gani Sheria na taratibu zetu zinakwaza uhuru huo na kwa pamoja tuchukue juhudi za kujenga mazingira hayo bora, miongoni mwa sheria zinazotumika vibaya kukwaza uhuru wa Habari ni sheria ya uchochezi.

Sambamba na hayo alisema alisema kuwa nchi nyingi ikiwemo Tanzania, zinafahamu umuhimu wa uhuru wa habari na ndio maana Katiba ya Jamhuri ya Muungano pamoja na Katiba ya Zanzibar katika Kifungu cha 18, zimeeleza kwa kina dhana na umuhimu wa uhuru wa Habari.

Kwamba kila mtu ana haki ya kutoa maoni na kujieleza, na kutafuta, kupokea na kusambaza habari na mawazo kupitia vyombo vyovyote vya habari bila ya kujali mipaka ya nchi“. Hata hivyo, tutakubaliana sote kwamba tunahitaji mashirikiano ya karibu ili kuhakikisha kwamba wananchi wanafaidi uhuru huo kwa kuondoa vikwazo vinavyoathiri utekelezaji wa maagizo hayo ya Katiba. 

Aidha alisema kuna haja ya makusudi kuwa na habari ambazo zinafuatiliwa na kufanyiwa uchunguzi badala ya kuwa na habari za matukio pekee. Maendeleo ya uhuru wa habari tunayoyaona leo kwingineko Duniani, ni matunda ya waandishi wenyewe kuonesha ubora wao na hivyo kutokuruhusu kuyumbishwa, hasa na wenye mamlaka ambao wanawajibika moja kwa moja kwa wananchi. 

Hivyo, katika hali kama hii, siyo rahisi viongozi kukiuka maadili na wakaachiwa pasi na hatua zinazostahiki; Na huo ndio uwajibikaji wa kweli; Kiongozi awajibike kwa wananchi na asiwe juu ya sheria.

Akieleza baadhi ya changamoto katika tasnia hiyo alisema wanahabari wanapaswa pia kujiongezea elimu na maarifa tukitambua kwamba hiyo ni katika misingi muhimu ya kujenga ufanisi wa kazi zenu na thamani yenu kwa jamii hasa katika mazingira ya sasa ya kidigitali pia ni vyema tukaweka azma ya kuzalisha habari ambazo tunazitafuta weyewe na siyo kutegemea kwa kiasi kikubwa taarifa za kudandia, maarufu kama habari za matukio.

Akifafanua zaidi alisema kwa udhati kabisa, juhudi hizi zote mlizochukua hazina budi kupongezwa na kuimarishwa, ambapo Serikali kwa upande wake itachukua hatua madhubuti katika kuhakikisha kuwa kunakuwepo na sheria rafiki za kada ya habari ili waandishi wa habari hapa nchini waweze kutekeleza majukumu yao katika mazingira bora zaidi.

Wakati hayo ya kijiri visiwani hapa wadau wa tasnia hiyo wanasema sharia ya habari inapaswa kutazamwa upya na kutengenezwa sharia ambayo itabeba maono ya walio wengi.

Mratib wa Baraza la Hahabari Tanzania kanda ya Zanzibar Shifaa Said alisema wananchi wengi wamekua na uelewa kuliko ilivyokua mika ya nyuma hivyo wanahitaji kujua mengi na kupambanua kila leo.

Alisema sharia inayoendelea kutumika sasa ilotungwa na kuanza kutumika mwaka 1988 imekosa vitu vingi vya msingi ambavyo anaamini kwa wakati huo havikuepo wala kuonekana umuhimu wake.

Akitolea mfano alisema ni matumizi ya teknolojia ambayo huku na kubadilika kila leo na kwamba kuna umuhimu mkubwa kuoneshwa kwenye sharia na kupewa nguvu ili wananchi walio wengi waweze kupata taarifa bila ya kubuguziwa.

 

 


Post a Comment

0 Comments