Na Ahmed Abdalla
Mkurugenzi wa Chama cha
waandishi wa habari TAMWA-ZNZ Dkt Mzuri Issa amesema vyombo vya habari
vinawajibu wa kujiwekea utaratibu na kuandaa vipindi maalumu ambavyo
vitaangazia haki ya uhuru wa kujieleza.
Aliyasema hayo wakati
alipokua akizungumza na waandishi wa habari katika mafunzo maalumu ambayo
yanalenga kuwakumbusha wanahabari visiwani Zanzibar jinsia ya kuthamini haki
hiyo muhimu.
Alisema tafaiti
zinaonesha kwa miaka mingi visiwani Zanzibar wanahabari wameisahau haki hio ya
kujieleza na kuwaacha wananchi wengi wakishindwa kupaza sauti zao.
Alisema iwapo vyombo
vya habari vitarudi na kujikita katika kutengeza vipindi na kuandaa habari
zinazohusu haki ya kujieleza vinaweza kuibua mengi ambayo yataweza kulisaidia
Taifa kwa ujumla.
Sambamba na hayo
Mkurugenzi huyo alisema iwapo uhuru wa kujieleza utatumia vyema unaweza pia
kuwakuza waandishi wa habari na kuvipa sifa zaidi vyombo vyao wanavyofanyika
kazi.
Kwa nyakati tofauti
baadhi ya washiri wa mkutano huo uliowezeskwa kwa mashirikiano na Internews
Tanzania walisema kwa muda mrefu wameisahau haki hiyo ya kujieleza.
Walisema kwa kusahau
huko wanadhani wamekosa kuwatendea haki wananchi wengi kila leo na ndio maana
sasa wameamua kuanza upya na kukusanya habari nyingi zitakazo husu haki ya
kujieleza.
Miongoni mwa wanahabari
hao ni Khatib Slemain alisema mara baadha ya kupata mafunzo hayo atajikita na
uandishi wa Makala zitakazowagusa zaidi watu na sauti zao.
0 Comments