Na Ahmed Abdulla
Mkurugenzi wa TAMWA-ZNZ
Dkt, Mzuri Issa amesema kwa miaka mingi Zanzibar imekua ikitumia sheria ya
habari ilioanza kufanya kazi tangu mwaka
1987 hadi sasa sheria ambayo imekua na chanagamoto nyingi kiutekelezaji.
Dkt, Mzuri aliyasema hayo
wakati alipokua akizungumza na wadau na wawakilishi wa vyombo mbalimbali vya
habari visiwani hapa katika mkutano malumu ulioandaliwa na TAMWA-ZNZ kwa
kushirikiana na Intenews Tanzania.
Alisema Zanzibar kama
sehemu ya Jamuhuri ya Muungano yenye sheria yake ya habari inapaswa kupiga
hatua ikiwemo kufanyia mabadiliko ya sheria hio.
Alisema katika dunia hii ya
utandawazi na uhitaji wa taarifa hadi sasa Zanzibar imekua ikinyima uhuru wa
habari kwa baadhi ya vipengele kwa mfano sheria imeweka wazi kuwa jeshi la
polisi linaweza kuzuia chapisho lolote lile iwapo watahisi kuna hali ambayo wao
haitawaridhisha.
Alisema jeshi la polisi na
taasisi nyengine hazipaswi kupewa uhuru wa kisheria kuminya uhuru wa kutoa na
kupata habari.
Kwa upande wake Mkurugenzi
mtendaji wa Hits Radio Hafidh Kassim alisema kumekua na vikwazo vingi katika
tasnia ya habari.
Alisema hadi sasa redio
nyingi Zanzibar zimekua zikifanya kazi kwa maelekezo aliyoadaia yanatoka juu
kwa baaadhi ya vipindi.
Alisema kuna wakati ukifika
vyombo vya habari hupelekewa hadi barua ya onyo wanapofanya vipindi vya
mahojiano na baadhi ya watu.
Nae katibu mtendaji wa
Klabu ya waandishi wa habari Pemba (PPC)Ali Mbarouk alisema mabadiliko ya
sheria ya habari ni kitu ambacho hakipaswi kuepukika kwa sasa.
Alisema sheria iliopo
imepitwa na wakati na kwamba kila inapochelewa kubadilishwa ni sawa na kuendelea
kuwakandamiza walio wengi.
0 Comments