Na Ahmed Abdulla
Mkurugenzi wa chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania
kwa upande wa Zanzibar TAMWA-ZNZ Dkt, Mzuri
Issa amepokea ugeni wa watu 14 kutoka Mataifa tofauti ulimwenguni, ugeni ambao
ulifika ofisi za Tunguu Wilaya kati Unguja.
Ugeni huo uliokua na lengo la kubadilishana uzoefu na
kujifunza jinsi ya TAMWA-ZNZ inavyofanya kazi kwa mafanikio makubwa katika
jamii.
Akizungumza na ugeni huo Dkt,Mzuri alisema ni sehemu ya
kujifunza na kubadilishana uzoefu ukizingatia miongoni wa wageni hao wanafanya
kazi katika mashirika tofauti yanayofanana katika utendaji wao wa kazi za kila
siku.
Alisema ni muhimu sana kubadilishana uzoefu juu ya mbinu
za kupambana na udhalilishaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto.
Pia alisema kuna changamoto katika mapambano ikiwemo
mila na desturi kwa baadhi ya wanafamilia kuendelea kuyaficha matendo ya
udhalilishaji wakihofia aibu.
Awali kiongozi wa msafara huo Anna-Keira alipongeza
juhudi kubwa inayofanywa na na chama hicho katika mapambano ya udhalilishaji.
Akaendelea kusisitiza zaidi na kusema ni muhimu juhudi
hizo kuendelezwa kwa sababu zinalenga kuwalinda wanawake na watoto kwa lengo la
kuhakikisha jamii inabaki salama.
0 Comments