Ticker

6/recent/ticker-posts

Maafisa Dawati La Jinsia Wataka Ufafanuzi Wa Kisheria Zuio La Dhamana Kwa Watuhumiwa Wa Ubakaji


 

Na Ahmed Abdulla Othman

Baadhi ya maafisa wa Jeshi la Polisi wanaofanya kazi katika madawati ya jinsia visiwani Zanzibar wamesema licha ya uwepo wa zuio la Rais la kutaka kutopewa dhamana watuhumiwa wa kesi za udhalilishaji lakini wamekua wakikabiliwa na chanagmoto ikiwemo ya kukosekana kwa maandiko ya kisheria.

 

Walioyasema hayo katika mkutano wa wadau wa kupambana na udhalilishaji ulioitishwa na TAMWA-ZNZ huko Tunguu Wilaya ya kati Unguja na kuwashirikisha wadau mbalimbali ikiwemo kutoka kisiwani Pemba.

 

Akitoa ushuhuda Afisa dawati la jinsia kutoka mkoa wa kusini Unguja Ali Mohamed Othman alisema wao kama maafisa wa dawati wanakutana na chanagmoto hizo ambazo kwa kukosa maandiko ya kisheria baadhi ya wakati huwawia vigumu.

 

Alisema ni hivi karibuni walipata taarifa za kubakwa kwa mtoto wa kike na wakamkamata mtu alietuhumiwa kufanya hivyo hatimae kumuweka ndani kama sehemu ya kazi zao lakini baada ya muda walipata barua ikiwataka wakajieleza kwanini wamemzuia mtuhumiwa huyo bila ya kumpa dhamana.

Alieleza hayo yote yalitokea akiamini ni kwa sababu sheria halisi ya zuio la dhamana haipo na ndio maana imekua ikitokea hali hiyo iwapo mtu atazuiliwa na kuwekwa ndania.

Wakati hayo yakijiri miongoni mwa washiriki wa mkutano huo akiwemo mzazi ambae ni miongoni mwa waliowahi kubakiwa mtoto wake alisema suala la dhamana kwa watuhumiwa linapaswa kuwekwa sawa na lisiachwe kwa kupitia tu kauli ya Rais.

Alisema kuna haja ya mabadiliko ya sheria na kifungu hicho kiwekwe wazi kuwa sheria inamzuia mtu yoyote anaetuhumiwa kufanya makossa hayo asipewe dhamana hadi pale uchunguzi utakapobainika na kisha hatua za kisheria kuchukuliwa.

Post a Comment

0 Comments