![]() |
Timu ya waandishi wa habari za michezo Zanzibar |
Timu ya waandishi wa habari za michezo
Zanzibar inayonolewa wa kaimu kocha mkuu Suleiman Nyanga jana Agosti 16, 2021 ilifanikiwa
kuitandika mabao 3-2 timu ya bodi ya mapato Zanzibar ZRB katika mchezo
uliochezwa majira ya saa 1:00 usikukatika uwanja wa Mao Tse Tung.
Magoli ya ZASWA FC yalifungwa na Is-haqa Mant,Kheir
Abdulkadir na Aboubakar Kharith P ambapo mabao yote hayo yalifungwa kipindi cha
kwanza huku mabao ya Timu ya ZRB yakifungwa na Lukman Kassim.
Mara baada ya ushindi huo kaimu kocha mkuu wa
ZASWA FC Suleiman Nyanga aliesema kikosi cha ZRB hakikuwa na ubora mkubwa wa
kuwafunga hasa katika kipindi cha kwanza hivyo kuwafanya kuongoza mabao hayo
matatu katika kipindi cha kwanza kizima.
“Hakika kikosi hakikuwa kizuri sana katika
mchezo wa jana ndio mana tulipata kuongoza bao 3-0 katika kipindi cha kwanxza”
alisema kocha huyo
Kocha huyo aliendelea kusema kuwa pia timu
yake ilifanya udhaifu katika kipindi cha pili hali iliyowarehusu ZRB kurejesha mabao mawili na ubao wa matokeo
ukasomeka 3-2.
“Kwa udaifu wa kikosi changu ulioufanya
kipindi cha pili kwa bahati mbaya tumerejeshewa mabao mawili na kuyafanya
matokeo kuwa 3-2” aliongezea kocha huyo
Alisema udhaifu wa kikosi chake umetokana na kutocheza
mechi kwa muda mrefu huku akisema ni takriban mwezi mmoja sasa timu haifanyi
mazoezi ambapo amesema ushindi huo umetokana na ari ya wachezaji,uzowefu wake
na benchi zima la ufundi pamoja na sapoti ya mashabiki.
Sambamba na hayo alisema anauongozi wa ZASWA
FC uandae utaratibu wa mazoezi ili watengeneze timu iliyo bora kwa ajili ya
ushindani zaidi.
Tokea timu ya ZAZWA ianze kunolewa na kocha
Nyanga imecheza michezo mitano ambapo imeshinda michezo mitatu na kupoteza michezo
miwili.
0 Comments