Ticker

6/recent/ticker-posts

"ITUMIENI SIKU YA WANAOJITOLEA DUNIANI KULETA MABADILIKO YA KIUCHUMI" WANZIRI OFISI YA RAISI TAMISEMI


 

Vijana nchini wametakiwa kuwa na utaratibu wa kujitolea katika mambo ya maendeleo ili kuisaidia serikani kuinua uchumi wa taifa.

Wito huo ulitolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi Tawala za mikoa, Serikali za mitaa na Idara maalumu za SMZ mhe, Masoud Ali Mohammed katika maadhimisho ya sherehe ya siku ya kujitolea duniani iliyofanyika huko katika hoteli ya Kendwa Rock.

Alisema vijana wana nafasi kubwa katika kuchangia maendeleo ya taifa hivyo endapo wa watajitolea katika kupiga vita rushwa,ubadhirifu wa mali za umma pamoja na vitendo vya udhalilishaji itapelekea ukuaji wa uchumi wa jamii na taifa kwa ujumla.

Aidha alisema Siku ya wanaojitolea duniani ni fursa adhimu kwa kila mmoja kuendeleza moyo wa kujitolea hivyo ameyaomba mashirika ya umoja wa mataifa jumuiya zisizo za kiserikali pamoja na serikali kuweza kuunga mkono juhudi za wale wanaojitolea na kutambua umuhimu wa michango yao wanayoitoa kwa Taifa.

Mwanaid Mohd ni mkurugenzi wa idara ya vijana na maendeleo amesema serikali itaendelea kuzithamini jitihada za vijana wanaojitolea kwani wana uwezo mkubwa wa kuchangia na kuleta mabadiliko ya kimaendeleo ya nchi.

Kwa upande wao  vijana wanaojitolea kutoka mashirika na tasisi mbalimbali wamesema Lengo la kujitolea ktk tasisi na mashirika hayo ni kuweza kuonesha watu wa makundi tofauti kuweza kupigania maendeleo ya taifa katika kuhakikisha wanaleta mageuzi ya kiuchumi katika jamii na taifa kwa ujumla.

Akitoa neon la shukurani mratibu mkaazi wa shirika la kujitolea la  umoja wa mataifa la UNV anayefanya kazi zake nchini Tanzania, bwana Christian Mwamanga ameishukuru serikali pamoja na wananchi wote kwa kushirikiana katika maadhimisho hayo huku akiwataka wananchi hao kuwa mabalozi wazuri kwa kuwaelimisha wananchi ambao hawakufika katika sherehe hizo umuhimu wa kujitolea katika taifa.

Siku ya wanaojitolea duniani hufanyika kila mwaka ifikapo tarehe 5 disemba na ujumbe wa mwaka huu ni kujitolea kwa pamoja unawaza.

Post a Comment

0 Comments