RAISI wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi
Dkt. Hussein Ali Hassan Mwinyi ametengua uteuzi wa katibu wa Raisi Bwana.
Suleiman Ahmed Saleh kuanzia leo Disemba 14.
Raisi Dkt. Mwinyi amefanya utenguzi huo kwa uwezo aliopewa
chini ya kifungu namba 53 cha katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 na kifungu namba
12(3) cha sheria ya utumishi wa umma namba 2 ya mwaka 2011.
Katka taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na
kutiwa saini na katibu wa baraza la mapinduzi ambaye pia ni katibu mkuu
kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee imesema kuwa Bwana. Suleiman atapangiwa
kazi nyengine.
Ikumbukwe mnamo Novemba 4 Dkt. Mwinyi alimteua bwana.
Suleiman Ahmed Saleh kuwa katibu wa Raisi wa Zanzibar.
0 Comments